Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka Atembelea Sinza Jijini Dar es Salaam na Kugundua Uuzaji Wa Maeneo Ya Wazi
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mkazi wa Sinza Ndahani Yohana ambaye amenunua eneo la wazi kwa utapeli kwa shilingi milioni 500 wiki mbili zilizopita, ambapo ramani halisi inaonyesha eneo hilo ni la wazi. Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E leo mchana. Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka wa pili kutoka kulia akiangalia ramani halisi inayoonyesha maeneo ya wazi wakati alipokagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi maeneo ya Sinza E wilaya ya Kinondoni, ambapo pia alikuwa akikagua mabango yaliyowekwa kwa ajili ya kuataarifu wananchi na kuwaelimisha maeneo ambayo ramani inaonyesha yako wazi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali. Diwani wa Sinza Bw. Renatus Pamba akimuonyesha Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi k...