Tunaweza kubishana mpaka asubuhi.Iweje,kwanini…mbona yule, hata mimi namjua nk.Lakini malumbano yetu yanaweza kuwa porojo tu kwani kwa mujibu wa Jarida maarufu la People la nchini Marekani, mwimbaji/mwanamuziki na mshindi wa tuzo kadhaa za Grammy,Beyonce Knowles(ukipenda Mrs.Jay-Z) ndiye Mwanamke Mzuri kushinda wote DUNIANI kwa mwaka 2012. Nimeweka neno duniani katika herufi kubwa kwa sababu binafsi huwa nina tatizo na wamarekani wanapoiona Marekani kuwa dunia. Ukiwaambia kwamba kuna mwanamke fulani mzuri sana yupo Tanzania au Kenya au Uganda watakushangaa.Hawaijui hivyo dunia unayoiongelea wewe. Beyonce ambaye ana umri wa miaka 30 sasa na Mama wa mtoto mmoja,Blue Ivy Carter, ameelezea kufurahishwa sana na heshima hiyo aliyopewa na Jarida la People. Wanawake wengine ambao wamewahi kushinda heshima hiyo ya People ni Michelle Pfeiffer, Julia Roberts, Nicole Kidman, Halle Berry, Jennifer Aniston, Angelina Jolie na Jennifer Lopez ambaye alishinda mwaka ja...