HARAIKI YA WANAFUNZI YAPAMBA SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANZANIA
Kati
ya wanafunzi hao, ni wanafunzi 727 ambapo 500 wanatoka Tanzania bara,
200 Tanzania visiwani na 27 ni mahodari wa kucheza sarakasi ambao
waliingia uwanjani na kutengeneza maumbo mbalimbali pamoja na kuimba
wimbo maalumu uitwao Uamuzi wa Busara.
Maumbo yaliyotengenezwa na haraiki hiyo ni pomoja na bendera ya taifa, herufi zenye umbo
la miaka 48 ya Muungano, na maumbo ambayo ndani yake walicheza
salakasi na ngoma za asili za ndalandala kutoka Tanzania bara na chaso
kutoka Zanzibar.
Maumbo
mengine ni pamoja na madini ya Tanzanaiti ambayo hayapatikani sehemu
yoyote duniani zaidi ya Tanzania na maumbo ya mazao ya uchumi ya katani
na pamba yanayolimwa Tanzania bara na karafuu Tanzania visiwani.
Haraiki
hiyo imeandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wakufunzi wake ni Kilema Athuman
Kambangwa akisaidiwa na Mwalimu Grace Ernest Kabohora kutoka shule ya
msingi Wailesi katika manispaa ya Temeke.
Comments
Post a Comment