Posts

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 YATANGAZWA

Tafadhali tizama matokeo hayo kwa ku: Bofya hapa = NECTA 2012 O Level Bofya hapa = NECTA 2012 O Level   Bofya hapa = NECTA 2012 O Level   Bofya hapa = NECTA 2012 O level Bofya hapa = NECTA 2012 QT ILANI: Link moja isipofunguka, jaribu nyingine, rudia tena na tena. Refresh page. Matokeo yote yapo kwenye tovuti ya NECTA ( www.necta.go.tz ). Leo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (Mb) ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kitaifa ya ya Kidato cha Nne, Maarifa na QT. Waziri amesema jumla ya watahiniwa waliofaulu ni  23,520 hali waliofeli ni 24,903. Shule bora kwa ufaulu zimetajwa kuwa  ni pamoja na St. Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Bagamoyo na Simini. Nyingine ni Kanosa, St. Jude na St. Mary. Source: http:// www.wavuti.com

AIKA & NAHREEL - USINIBWAGE (Official Video)

Image

DOWNLOAD NGOMA YA DIAMOND FT TANZANITE INAITWA MAPENZI

Ripoti Maalum:Wizi wa fedha katika ATM ulivyofanyika

Image
KUKUA kwa teknolojia za fedha ambako kumerahisisha ufanisi wa matumizi na utunzaji fedha, kunaonekana kugeuka kuwa balaa kutokana na kuibuka kwa wizi wa fedha zilizohifadhiwa kwenye akaunti za wateja. Taarifa za wizi huu zilianza kurindima Machi 2010 na Sh300 bilioni ziliibwa kwa njia ya mtandao  kupitia mashine za ATM,   kati ya kiasi hicho Sh360 milioni zikihusisha benki moja ya NBC. Hata hivyo, mwaka huo walikamatwa watu wanne baada ya kuripotiwa wizi huo mkubwa, sambamba na taarifa za kukamatwa kwa watu hao alikamatwa mfanyabiashara mmoja aliyefanya jaribio la kuiba  Sh221 milioni kutoka Benki ya NBC. Wimbi la wizi huo limeibuka tena Oktoba mwaka jana hadi Februari mwaka huu, inakadiriwa Sh700 milioni zimeibwa Benki ya NMB na benki zingine kwa nyakati tofauti. Tayari, polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu wanne ambao wanadaiwa kukutwa wakiwa kwenye mpango wa kuendelea kuiba fedha ndani ...

TAARIFA YA INSPEKTA JENERALI WA POLISI SAID MWEMA KWA UMMA

Image
Source: http:// www.wavuti.com/#ixzz2LEKkhJaW

Chuo cha St John’s chafungwa baada ya Wanafunzi kususia mtihani wakipinga manyanyaso ya Wahadhiri

Chuo Kikuu cha St John’s cha mkoani Dodoma kimefungwa baada ya wanafunzi kususia mitihani wakituhumu na kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na wahadhiri kwa kuwangusha kwenye mitihani na baadhi kuwabaka wanafunzi wa kike. Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Gabriel Mwaluko, wanafunzi zaidi ya 290 wamesimamishwa masomo baada ya kukiuka sheria na kugomea mitihani, hivyo chuo kimefungwa kikisubiri taratibu za kinidhamu kuchukuliwa. Awali uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo ulieleza kuwa wanafunzi 290 wa St John’s na vyuo vikuu vishiriki vya Dar es Salaam walisimamishwa masomo huku uongozi wa chuo ukiwapa barua za kuwaondoa chuoni kuanzia wiki hii. Habari hizo zilisema wanafunzi 196 wanaosoma Dodoma na wengine 94 wanaosoma katika vyuo vishiriki vya St. Mark's na Town Centre vya jijini walipewa barua za kuondolewa chuoni. Rais wa serikali ya wanafunzi, Andrew Chiduo, akizungumza na NIPASHE Jumapili, alisema hatua ya kuwasimamisha inalenga kuwatisha ili kuendelea kuwal...

GOLDIE AMBAYE NI MCHUMBA WA PREZZO AFARIKI DUNIA

Image
Yule Mwanadada kutoka Nigeria aliyeshiriki katika Big Brother Africa Star game 2012 na baadaye kuanza mahusiano ya kimapenzi na rapper wa Kenya Prezzo, amefariki dunia. Msanii huyo aliyeimba nyimbo ya Skibobo, akiwa amemshirikisha AY, aliaga dunia mapema jana, muda mfupi tu baada ya kurudi akitokea Marekani alipokua ameenda kushuhudia tuzo za Grammys. Goldie, inasemekana aliugua ghafla na hapo hapo kufariki. Meneja wa msanii huyo alidhihirisha habari hizi kupitia account ya twitter ya Goldie kwa kusema;  Tumejaribu kupata mawasiliano na Prezzo atoe tamko, lakini hatujafanikiwa. Tunatoa pole kwa Prezzo, familia ya Goldie Harvey, wasanii wenzake pamoja na fans wa mwanadada huyu. source www.freebongo.blogspot.com