Ripoti Maalum:Wizi wa fedha katika ATM ulivyofanyika



KUKUA kwa teknolojia za fedha ambako kumerahisisha ufanisi wa matumizi na utunzaji fedha, kunaonekana kugeuka kuwa balaa kutokana na kuibuka kwa wizi wa fedha zilizohifadhiwa kwenye akaunti za wateja.


Taarifa za wizi huu zilianza kurindima Machi 2010 na Sh300 bilioni ziliibwa kwa njia ya mtandao  kupitia mashine za ATM,   kati ya kiasi hicho Sh360 milioni zikihusisha benki moja ya NBC.
Hata hivyo, mwaka huo walikamatwa watu wanne baada ya kuripotiwa wizi huo mkubwa, sambamba na taarifa za kukamatwa kwa watu hao alikamatwa mfanyabiashara mmoja aliyefanya jaribio la kuiba  Sh221 milioni kutoka Benki ya NBC.
Wimbi la wizi huo limeibuka tena Oktoba mwaka jana hadi Februari mwaka huu, inakadiriwa Sh700 milioni zimeibwa Benki ya NMB na benki zingine kwa nyakati tofauti.
Tayari, polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu wanne ambao wanadaiwa kukutwa wakiwa kwenye mpango wa kuendelea kuiba fedha ndani ya mashine za kuchukuliwa fedha (ATM) za Benki ya NMB tawi la PPF Plaza,   saa 6:00 usiku.
Kunaswa kwa watu hao kunatokana na mtego baina ya maofisa wa benki na polisi uliofanikisha Februari 10 mwaka huu, kumtia mbaroni mtuhumiwa mmoja akiwa katika  ATM ya NMB katika tawi la PPF Plaza, akiingia kuchukua fedha ambaye alifanikisha kunaswa kwa watuhumiwa wengine na vifaa vinavyotumika kwa wizi huo.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Christopher Fuime alieleza kuwa baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo alifanikisha kukamatwa wengine, ikiwamo vifaa mbalimbali ambavyo wamekuwa wakivitumia kufanyia uhalifu huo.
“Kwa muda mrefu sasa tulikuwa tukihangaika  na wahalifu wa aina hii, kwani tangu mwaka Oktoba mwaka jana tumekuwa tukipokea kesi mbalimbali za wizi wa fedha katika akaunti zao, lakini tumefanikiwa juzi kuwatia mbaroni,” alisema.
Tangu kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao, idadi ya malalamiko ambayo wastani wa kesi 15 walizokuwa wakipokea kwa siku 14 zimeisha, hali ambayo inawafanya kuamini kuwa wahusika hao walikuwa vinara wakuu wa wizi huo.
“Hatuna maana kwamba kukamatwa kwao uhalifu huu utapungua,  wizi huu una mtandao mpana kwa vile hata wahalifu hao wamedokeza wamekuwa wakifanya uhalifu huo kwa kushirikiana na wataalamu wa kompyuta kutoka nchini Bulgaria,” alisema.
Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa vilivyokamatwa ni  kadi bandia za kuchukulia fedha katika ATM 194 za Banki ya NMB, kati yake kadi 95 zilikuwa na namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina na picha ya mtu anayedaiwa ni mtumiaji, kadi zingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti namba 5068000322 zikitumia jina lingine na picha moja.
Pia, walinasa kadi za Benki ya DTB 36, ambazo kati yake 18 zilikuwa na jina moja la Kelvin G. Gratias zikiwa namba  20497883, kadi 12 zikitumia jina lingine na akaunti namba 2049783, huku kadi sita zikitumia jina la mtu mwingine akaunti namba 2049783.
Kadi zingine tatu zenye maandishi ya Download List na nyingine ikiwa ni kadi ya visa ya Benki ya KCB yenye namba 4183546040003827 zikitumia jina moja, kadi zingine zilikuwa ni tupu zisizo na maandishi wala nembo ya benki yoyote na nyingine zikiwa na nembo ya Soviet Royality, kadi ya raia wa Urusi ikiwa na namba Sand 000724.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA