Posts

KATUNI YA LEO................HATARI TUPU

Image
Rais Jakaya Kikwete amekemea vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote, “Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete. Rais alisema wote waliohusika na vurugu hizo, Serikali itawasaka ikiwa ni pamoja na viongozi wa vurugu hizo na ili kuwawajibishwa: “Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.” Source:  http://www.wavuti.com/#ixzz2U6Em1STi

BUNGE LIMEHAIRISHWA TENA MPAKA KESHO SAA 3 ASUBUHI.

Image
Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Anna Makinda amehairisha Bunge mpaka kesho saa 3 asubuhi ,ili Kamati tofauti za bunge zikajadili kuhusu hali inayoendelea huko mkoani Mtwara

DOWNLOAD NA KUSIKILIZA WIMBO MPYA WA MALFRED- "PIGANA"

HAPPY BIRTHDAY CLASSMATE ONESMO FAUSTINE

Image
wish all da best in ur life bro

Msanii Joseph Haule (Prof. Jay) ajiunga CHADEMA

Image
what I expected have become true......ndani ya GWANDA.

TANGAZO KUTOKA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu  wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi, Mei 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kitaanza  rasmi tarehe 1 Julai, 2013 kwa ada ya Shilingi 35,000/=. Kipindi cha malipo  bila adhabu kitaishia tarehe 31 Agosti, 2013. Kuanzia tarehe 1 Septemba, 2013 hadi tarehe 30 Septemba, 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya  Shilingi 50,000/- (ada pamoja na faini). Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti: www.necta.go.tz. ya Baraza la Mitihani la Tanzania. Kabla ya kujisajili  kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani  kuchukua namba rejea (reference number) watakazotumia kujisajili.  Hakuna  mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kupata namba rejea kutoka katika kituo  anachokusudia kufanyia Mtihani. Wakuu wote wa vituo nchini watakabidhiwa  namba reje...

WASANII WATAKAOTUMBUIZA KATIKA SHOW YA UFUNGUZI WA BIG BROTHER WATAJWA

Image
Show ya ufunguzi wa msimu mpya wa shindano la Big Brother Africa itafanyika Jumapili hii, May 26 nchini Afrika Kusini.  Usiku huo utawaonesha washiriki wote 28 watakaoanza safari ya miezi mitatu ya kuzisaka dola laki tatu za msimu wa nane wa Big Brother Africa, The Chase. Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye ufunguzi huo ni pamoja na STL wa Kenya, Don Jazzy, D’ Prince na Wande Coal kutoka Nigeria na kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini. Pia mchekeshaji wa Kenya Daniel Ndambuki, maarufu kama Churchill atapanda kwenye stage kuwavunja mbavu watazamaji wa show hiyo katika nchi 50 barani Afrika.  Show hiyo itaonekana live pia kupitia website ya Big Brother