KATUNI YA LEO................HATARI TUPU
Rais Jakaya Kikwete amekemea vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote, “Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete.
Rais alisema wote waliohusika na vurugu hizo, Serikali itawasaka ikiwa ni pamoja na viongozi wa vurugu hizo na ili kuwawajibishwa: “Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.”

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2U6Em1STi
Comments
Post a Comment