TANGAZO KUTOKA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu
wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi, Mei
2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kitaanza
rasmi tarehe 1 Julai, 2013 kwa ada ya Shilingi 35,000/=. Kipindi cha malipo
bila adhabu kitaishia tarehe 31 Agosti, 2013. Kuanzia tarehe 1 Septemba,
2013 hadi tarehe 30 Septemba, 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya
Shilingi 50,000/- (ada pamoja na faini).
Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti:
www.necta.go.tz. ya Baraza la Mitihani la Tanzania. Kabla ya kujisajili
kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani
kuchukua namba rejea (reference number) watakazotumia kujisajili.
Hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kupata namba rejea kutoka katika kituo
anachokusudia kufanyia Mtihani. Wakuu wote wa vituo nchini watakabidhiwa
namba rejea hizo kabla ya muda wa usajili kuanza na watazigawa kwa
watahiniwa tarajali bila malipo.
IMETOLEWA NA:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZA
Comments
Post a Comment