SWAHILI FASHION WEEK YA SITA YAZINDULIWA WABUNIFU 40 KUONESHA KAZI ZAO DAR ES SALAAM
Maonesho ya sita ya Swahili Fashion Week yatafanyika Golden Tulip Hotel kuanzia tarehe 5 mpaka 8 Desemba 2013, Dar Es Salaam, Tanzania. Swahili Fashion week 2013 itakusanya wabunifu 40 kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuonesha mitindo yao, yenye kwenda na wakati na kutegemewa kushika soko la Afrika Mashariki mwaka 2014. “Swahili Fashion Week mwaka huu ina lengo la kuifikia jamii zaidi, na kukuza vipaji katika tasnia ya mitindo. Ni zaidi kuhusu kuthamini wabunifu wa kwetu na kuwatengezea jina,huku tukiwapeleka ngazi za juu zaidi kila mwaka” Akizungumza Bw. Washington Benbella, Meneja wa Swahili Fashion Week Ukiwa ni mwaka wa 6 wa Swahili Fashion Week, Katika mashindano ya wabunifu wanaochipukia, Waandaaji wamependekeza dhima ya mwaka huu (theme) “Evolution” ambayo inawataka wabunifu chipukizi hao kubuni mavazi yanayoashiria mabadiliko, si lazima upya, ila yenye muonekano wa kitofauti na mzuri. “Tunasisitiza jamii iunge mkono tasnia ya mitindo na kuvaa mavazi ya kik...