KARIBU KATIKA KONGAMANO KUBWA LA AFYA NA MAHUSIANO LITAKALOFANYIKA KATIKA CHUO CHA SAUT: JUMAMOSI HII



Jumamosi tar.19/10/2013 kutakuwa "KONGAMANO KUBWA LA AFYA NA MAHUSIANO" litakalofanyika katika Chuo Kikuu Cha St.Augustine, ukumbi wa M13 kuanzia saa tatu (03) asubuhi hadi saa saba (07) mchana.
Mgeni Rasmi ni Waziri wa Afya Mh.Husein Mwinyi,mgeni Maalumu ni Mh.James Mbatia (Mbunge na Mwenyekiti wa asasi ya Utu-Mtanzania)

Kongamano hili lilikuwa liende sambamba na uzinduzi wa Kitabu kiitwacho “TUMAINI LANGU, ELIMU YANGU”kilichoandikwa na Godlisen Malisa aliyekuwa rais wa chuo mwaka 2012-2013.

Kongamano hili nimeandaliwa mahususi kutoa nafasi kwa vijana wasomi kujadili kuhusu afya zao, mahusiano yao, na hatari ya maambukizi ya VVU kwa wasomi wetu.

Kongamano litajumuisha uwasilishaji wa mada zilizofanyiwa utafiti wa kina juu ya MAHUSIANO HATARISHI yanayoweza kupelekea maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa vijana wasomi.

Karibu uje ukutane na Waziri mwenye dhamana ya Afya uweze kuuliza mambo yote muhimu kuhusu wizara yake.

Karibu ukutane na mwanaharakati James Mbatia, akuelimishe na kukufundisha umuhimu wa Elimu yako na namna ya kuepuka maambukizi hatarishi. Karibu utoe maoni, uulize maswali, uchangie hoja etc.

Kongamano litajumuisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya kanda ya ziwa ikiwemo CBE, IJA, DIT, TIA, OPEN University, Chuo cha waalimu Butimba, Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Bugando, Chuo cha Uuguzi Bukumbi, Chuo cha Uvuvi Nyegezi, Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt.Meru Mwanza campus, nk.

Kwanini vijana wengi wasomi wanajiiingiza katika Mahusiano hatarishi? Ni kweli kuchelewa kwa “boom” kunachangia mabinti wasomi kujiuza? Je ni kweli WATOTO WA MAMA SALMA wapo vyuoni? Je haiwezekani kuwa na mpenzi mmoja kuanzia First year hadi third year? Etc.

Hayo na mengine mengi utayapata ukihudhuria Kongamano hili la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika nchini hasa kanda hii ya ziwa.

Mada zitawasilishwa na wahadhiri kutoka chuo kikuu cha SAayansi ya Tiba Bugando na Chuo Kikuu SAUT.

Pia kongamano hili litafungua rasmi mashindano ya uandishi wa Insha juu ya sababu za wasomi wa vyuo vya elimu ya juu kujiingiza katika mahusiano hatarishi na suluhisho lake. Mshindi katika uandishi wa Insha atazawadiwa Sh.200,000/= Taslimu.

Burudani zitakuwepo za kusisimua na tragicomedy za kuelimisha pia zitakuwepo.

Vyombo mbalimbali vya habari vitakuwepo, ikiwa ni pamoja na ITV, StarTv, na magazeti mbalimbali. Radio SAUT Fm watarusha kongamano hilo na baadae litarudiwa kwenye vipindi vya usiku, kwa wale watakaoshindwa kusikiliza mchana.

Shukrani za dhati ziende kwa Uongozi wa Chuo cha SAUT, Radio SAUT Fm, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Asasi ya Utu Mtanzania, Shirika la Pensheni kwa watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Moil Petroleum, AprilMey Entertainment, Wizara ya Afya na Mazingira SAUTSO na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine wamefanikisha kuandaa kongamono hili.

Shukrani pia zikufikie wewe utakayesoma hapa na kuhamasisha wenzio kushiriki. Fikisha taarifa hizi kwa watu wengi kadri uwezavyo. Pia Jitahidi sana kuwahi ili usikose nafasi.! Ukipata ujumbe huu wajulishe wenzio

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA