SWAHILI FASHION WEEK YA SITA YAZINDULIWA WABUNIFU 40 KUONESHA KAZI ZAO DAR ES SALAAM



Maonesho ya sita ya Swahili Fashion Week yatafanyika Golden Tulip Hotel kuanzia tarehe 5 mpaka 8 Desemba 2013, Dar Es Salaam, Tanzania.

Swahili Fashion week 2013 itakusanya wabunifu 40 kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuonesha mitindo yao, yenye kwenda na wakati na kutegemewa kushika soko la Afrika Mashariki mwaka 2014.

“Swahili Fashion Week mwaka huu ina lengo la kuifikia jamii zaidi, na kukuza vipaji katika tasnia ya mitindo. Ni zaidi kuhusu kuthamini wabunifu wa kwetu na kuwatengezea jina,huku tukiwapeleka ngazi za juu zaidi kila mwaka” Akizungumza Bw. Washington Benbella, Meneja wa Swahili Fashion Week

Ukiwa ni mwaka wa 6 wa Swahili Fashion Week, Katika mashindano ya wabunifu wanaochipukia, Waandaaji wamependekeza dhima ya mwaka huu (theme) “Evolution” ambayo inawataka wabunifu chipukizi hao kubuni mavazi yanayoashiria mabadiliko, si lazima upya, ila yenye muonekano wa kitofauti na mzuri.

“Tunasisitiza jamii iunge mkono tasnia ya mitindo na kuvaa mavazi ya kikwetu, hasa kwa Tanzania. Vipaji vya nyumbani vinahitaji kukuzwa ili kufikia majina yanayotambulika duniani katika tasnia hii. Hisani huanza nyumbani, na ndio maana tunategemea kampuni pamoja na mashirika mbali mbali kusaidia tasnia ya mitindo” Hamis K Omary, Meneja Masoko Swahili Fashion Week.
Swahili Fashion week imedhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel, Eventlites, Push Mobile, BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa), Ultimate Security, Global Outdoor Ltd na 361 Degrees.

KWA MAWASILIANO: Kauthar Ally, Media & PR Manager
SIMU: +255-718 855 590


Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo


Bw. Honest Arroyal,Mratibu wa Mitindo Swahili Fashion Week (Kulia) na Catherine Lumbanga, Mratibu wa Masoko Golden Tulip Hotel wakizungumzia ujio mpya wa Swahili Fashion Week 2013


Happy Shame, (Kulia) Meneja Masoko wa EATV na Ea Radio akizungumzia mipango ya EATV na Radio juu ya Swahili Fashion Week mwaka huu


Meneja Maboresho Swahili Fashion Week, Hamis K Omary akizungumzia uboreshwaji wa Swahili Fashion Week 2013


Meneja Maboresho wa Swahili Fashion Week Hamis K Omary akijibu maswali kutok kwa waandishi wa habari

Meneja wa Swahili Fashion Week Washington Benbella (Katikati)akizungumzia tarehe za Swahili Fashion Week



Mratibu wa Masoko na Mauzo kutoka Hoteli ya Golden Tulip Bi. Catherine Lumbanga akizungumzia jinsi  hoteli yao inafurahi kushirikiana Swahili Fashion Week kwa mwaka wa pili mfululizo


Mkutano na waandishi wa Habari kuzindua Swahili Fashion week



Mkutano na waandishi wa Habari kuzindua Swahili Fashion Week

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA