BALOTELLI ASAINI MIAKA MITATU LIVERPOOL
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan kutua Liverpool kwa Mkataba wa miaka mitatau. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliwasili Melwood leo mchana kukamilisha uhamisho wake kabla ya kwenda kufanya mazoezi maalum na mkuu wa idara ya kuwaweka fiti wachezaji, Ryland Morgans. Nyota huyo wa zamani wa Manchester City atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 125,000 kwa wiki Anfield na atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya timu yake hiyo ya zamani usiku wa leo. Pamoja na kusaini mkataba wa miaka mitatu, Balotelli anaweza kuongezewa mwaka mmoja kwa mujibu wa kandarasi hiyo. Chanzo:Bongostaz