EPUKA UTAPELI HUU UNAOZIDI KUOTA MIZIZI KATIKA MAKUNDI YA KIBIASHARA NDANI YA FACEBOOK



Teknolojia imekuwa ikizidi kubadilisha maisha yetu kuwa rahisi zaidi, “biashara kwa njia ya mtandao” sio sentensi geni tena masikioni mwetu kwa nyakati hizi za kidijitali, hii imepelekea kampuni, benki, Ngo’s, Saccos wafanyabiashara kutafuta nafasi ya kuingia kwenye world wide website yaani www ili kutengeza nafasi mpya ya kujitangaza,kupanua wigo wa hutoaji huduma na kurahisisha upatikanaji wa huduma zao kwa njia ya internet. kuna makampuni makubwa duniani ambayo yanategemea kujiendesha kibiashara kwa kutegemea njia ya internet kufanya biashara yake, mfano ebay, amazon, Alibaba, iTunes, beforward nk.


Katika kila jambo zuri, baya haliwezi kukosekana, katika mtandao wa facebook kumekuwa na ongezeko la kasi la utengenezaji wa vikundi maarufu kama (facebook Group) ambapo watu wenye mtizamo na malengo ya aina moja wanakutanishwa katika kikundi kimoja. Kundi hilo linaweza kuwa la kibiashara, vipindi vya redio au Luninga, habari, siasa, mahusiano, dini, michezo, Sanaa, wataalamu wa fani moja, kikundi cha watu wa ukanda au kabila fulani, shule n.k

Nimekuwa mfatiliaji mzuri hasa wa makundi ya kibiashara ndani ya facebook ambapo muuzaji na mnunuzi wanakutana kwa njia ya mtandao na hatimaye wanaweza kukutana uso kwa uso pindi wanapokubaliana kulingana na makubaliano wanayoweza kuafikiana kwenye bidhaa au huduma anayoitoa muuzaji. Facebook group ambazo nimekuwa nikifuatilia zaidi ni Biashara Dar, Uza & nunua online shop, Dar Phone Deals,  Dar Largest Trade centre, Deals in Dar, Deals in East Africa,  Dar Selling and Buying Deals. Biashara ambazo zimekuwa zikitawala Zaidi katika makundi haya ni simu na vifaa vyake, laptop, kamera, uuzaji wa magari, dawa za kupunguza unene, uzito, vitambi, biashara ya urembo, nguo, vifaa vya umeme, ujenzi nk.

Faida ni nyingi zinazopatikana kwa kutumia makundi ya facebook yaliyo katika mlengo wa kibiashara, kama sehemu ya kutangaza bidhaa au huduma ambayo mjasiliamali, au kampuni Fulani inatoa na kuweza kusambaza taarifa kwa maelfu ya watu na kuweza kupunguza gharama za kutumia njia kama radio, television au gazeti katika kutangaza bidhaa au huduma hiyo. Facebook group imekuwa msaada kwa wanakikundi wenye mawazo ya kibiashara (business idea) kwa wale ambao hawajui wanaweza kuanza vipi mpaka kufikia malengo wanayoyakusudia lakini kupitia makundi anaweza kuweza kupata ufafanuzi, mawazo kutoka kwa wanakikundi na jinsi ya kufanya ili kufikia malengo.

Watu wengine wanapata taarifa za  bidhaa au huduma fulani za kibiashara wanazozihitaji kwa kuulizia wanakikundi wenzao na kuweza kuzipata kirahisi zaidi lakini pia lipo jambo lingine zuri la kuweza kupata bidhaa unayoipenda mpaka mahali ulipo itategemeana na makubaliano yatakayofanyika baina ya muuzaji na mnunuzi.

Pamoja na kutizama katika mazuri mengi yaliyopo katika kutumia makundi ya kibiashara ndani ya facebook hiki ndicho Kinachonisukuma kuandiki habari hii, baada ya kuona watu wakilalamika juu ya utepeli ambao umezidi kuongezeka kila kukicha. Juzi wakati nikipitia post mbalimbali katika makundi haya nikakutana na huyu mdau ambaye anatumia jina la Aqeel Dhall baada ya kupigwa changa la macho pale maeneo ya T.M.J hospitali, hisia na wazo likaja kichwani kuandika na kuwapa taarifa wengine ambao hawajakutana na mkasa kama wa ndugu Aqeel Dhall ambaye anakuwa kama mfano wa kumtumia katika kundi la watu wengine ambao wameshalizwa au wako mbioni kulizwa kwa style kama hii hivyo kuwa makini kwa biashara hizi za kimtandao.
Aqeel DhallDeAlS iN DaR
19 August at 21:41 ·
I think this is pretty much getting serious now. I was selling my Note 3 and was called up by this dude. I said if we could meet opposite T.M.J hospital, he said that he works at Tanesco. I agreed to go there and when we met, he took me into his "so called office" and told me to wait outside as he was gno show the phone to his boss. I made a HUGE mistake by giving him the phone. What made me give my phone to him was his appearance (Tie suited guy). The door inside had a leading to the exit and he ran away with my phone. I cannot get the phone back I know because I had factory reset my phone but just as a fellow friend, I would request all members to please take care before selling your items to strangers.
It was on 16th of Aug 2014, Sat
His number was or maybe is: 0719 199455.
And he said that his name was Japhet.
Black (no racist) guy, and he applied propper perfume which obviously doesn't portray his cheap quality. If at all, you come to know this guy or have a clue.. just call or whatsapp on 0753 188855.
Beware!!! “

Njia za kuepukana na utapeli huu.
1. Tafadhari akikisha kwanza bidhaa inayouzwa inaendana na zile sifa alizozitoa muuzaji kwenye post yake mtandaoni kabla haujatoa pesa kulipia bidhaa, je sifa zinaendana?

2. Msiuziane bidhaa kienyeji, pendelea kuwa na watu wengine kama mashahidi wakati wa kuuziana bidhaa ikiwezekana fuata sheria za kuuziana mali ili kujiweka katika mikono salama.

3.  Unaponunua simu tafadhali itoe kwanza betri ndo uiwashe, wengine utegesha kumbe chaji kimeo au network haipandi.

4. Usikubali mnunuzi kuchua bidhaa yako kwenda kuonyesha mtu wake wa karibu kama mchumba, boss n.k kabla ya kutoa pesa hapa ndipo wengi wanalizwa na kuachwa.

5.Usimwamini mtu kwa kumwangalia alivyovaa na kudhani ndio mwaminifu mara nyingi matapeli wanakuwa smart ili usiweze kuwagundua kirahisi.

  6.Kuwa makini na maeneo ya kwenda kufanyia hiyo biashara pamoja na muda husika ambao deal inaenda kufanyika.

Imeandaliwa na Nyanja Kelvin Poti
WhatsApp 0715 01 9393
E-mail kelvinnyanja@gmail.com




Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA