UFARANSA YAVUNJA SERIKALI YAKE
Rais wa Ufaransa Francois Hollande akitoa hotuba huko katika jumba la Elysee
Rais wa
Ufaransa Francois Hollande amevunja serikali yake. Waziri Mkuu Manuel
Valls amewasilisha hati za kujiuzulu kwa serikali yake ya kisoshalisti
Jumatatu na Bw. Hollande amekubali na kumwamuru waziri mkuu huyo kuunda
serikali mpya ifikapo Jumanne.
Hatua
hiyo ya kisiasa inafuatia ukosoaji wa Waziri wa Uchumi Arnaud Montebourg
juu ya sera za uchumi za nchi hiyo na kuhoji juu ya hatua
zilizochukuliwa kwa upande wa bajeti na mshirika wao Ujerumani.
Ufaransa
iko kwenye msukumo mkali kutoka Umoja wa Ulaya juu ya kurekebisha mfumo
wake wa kifedha lakini Montebourg amehoji kama kubana huko matumizi
kunakoshinikizwa na umoja wa Ulaya kutakuwa na faida yeyote kwa
Ufaransa.
CHANZO:VOA
Comments
Post a Comment