LULU, WOLPER WAONESHANA JEURI YA MABWANA
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Walper. Sakata la kupangishiwa nyumba za kifahari na wanaume linazidi kuchukua sura mpya kwa mastaa wa kike ndani ya tasnia ya sinema za Kibongo ambapo safari hii mastaa wawili, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper ‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja ambao awali walikuwa juu wakipotezwa. Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. TAMBO ZA NANI ZAIDI? Uchunguzi wa Ijumaa umebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko wengine. Ilidaiwa kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba la kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa kupangishiwa mjengo wa maana na bwana’ke uliopo maeneo hayohayo. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu amb...