Posts

MOAT yaunda kamati kupinga muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari kujadiliwa

Image
ubi Nukta 5/26/2015 09:54:00 PM No Comment Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto) na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari. Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini, MOAT , kimeunda kamati ambayo itaenda mjini Dodoma kwa ajili ya kupinga kujadiliwa bungeni muswada wa sheria za vyombo vya habari. Akizungumza jijini Dar es Salam mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi amesema muswada huo unakandamiza haki na uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki ya wananchi kupata habari jambo ambalo linanyima demokrasia katika vyombo vya habari hivyo. Dk. Mengi amebainisha kuwa ni wakati sasa kwa vyombo vya habari kuweza kupiga kelele juu ya ubovu wa muswada huo ambao unatarajia kuwasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na katika kufanikisha hilo watatoa elimu kwa wabunge kuhusiana na muswada huo unavyokandamiza uhuru wa habari. Mengi amesema vipengele v...

MAGAZETI YA LEO JUMATANO, MEI 27 SOMA HAPA

Image

MAMBO 10 ALIYOZUNGUMZA LOWASSA NA WAANDISHI WA HABARI KWA MARA YA KWANZA

Image
Mhe. Edward Lowassa amefanya mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma ambapo ananukuliwa kusema yafuatayo kwa muhtasari: 1. Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii. 2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa ni waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo Aliekuwa DC Igunga Elibariki Kingu. Pia aliyekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki naye alikuwepo. Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo gani na kwan...