MOAT yaunda kamati kupinga muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari kujadiliwa

5/26/2015 09:54:00 PM
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto) na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari.

Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini, MOAT , kimeunda kamati ambayo itaenda mjini Dodoma kwa ajili ya kupinga kujadiliwa bungeni muswada wa sheria za vyombo vya habari.

Akizungumza jijini Dar es Salam mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi amesema muswada huo unakandamiza haki na uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki ya wananchi kupata habari jambo ambalo linanyima demokrasia katika vyombo vya habari hivyo.

Dk. Mengi amebainisha kuwa ni wakati sasa kwa vyombo vya habari kuweza kupiga kelele juu ya ubovu wa muswada huo ambao unatarajia kuwasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na katika kufanikisha hilo watatoa elimu kwa wabunge kuhusiana na muswada huo unavyokandamiza uhuru wa habari.

Mengi amesema vipengele vilivyotumika katika mswada huo ni wazi vinataka kuuwa tasnia ya habari pamoja na ajira kwa waandishi wa habari jambo ambalo sio njema kwa taifa.

Serikali imeandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha bajeti kinachoendelea mjini Dodoma ili kujadili miswada ya sheria.



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA