Posts

Taarifa ya maamuzi 6 ya NEC: Watakaoruhusiwa na Watakaozuiliwa kupiga kura

Image

Marekebisho ya NEC 22.10.2015 ya Ratiba ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu

Image

JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI SIKU YA KUPIGA KURA

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari jana (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jam...

Mahojiano maalumu: Lowassa @AzamTv - Afya, Tuhuma, Kampeni

Uchambuzi wa NIPASHE kuhusu ahadi za wagombea Urais Tanzania 2015

Image
Huku zikiwa zimebaki siku 10 kabla ya kufikiwa kwa siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, wagombea urais wanaochuana kwa karibu kutokana na wingi wa watu wanaojitokeza katika kampeni zao, Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaendelea kutoa ahadi nzito kadhaa kwa wapiga kura. Kadiri inavyoonekana, ahadi hizo zikitekelezwa kwa asilimia 100, zitafanya muujiza kwa kuibadili Tanzania kutoka katika hali duni ya upatikanaji wa baadhi ya huduma za jamii na kuonekana kama `Ulaya'. Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kwa wiki kadhaa tangu kampeni za uchaguzi mkuu kuanza rasmi Agosti 22, mwaka huu, umebaini kuwa hadi sasa, Magufuli na Lowassa wameshatoa ahadi nyingi nzito na ambazo zikitekelezwa kwa ukamilifu pindi yeyote kati yao akishinda zitaibadili kwa kiasi kikubwa Tanzania itakayoachwa na serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Uchunguzi huo wa Nipashe pia umebaini kuwa kati ya ahadi zote, zipo tano zinaz...

DK MAGUFULI ASHIRIKI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU DK KIGODA DAR

Image
 Mke wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Janeth Magufuli (kulia) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe.Mwantum Mahiza wakiwa wamemshikilia mke wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.  Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda, Omary Abdallah Kigoda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (kulia) akizungumza na Binti wa Marehemu Amina Kigoda ,katikati ni mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza. Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimpa pole mke wa marehemu.  Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na...

Tanzia! Dk Makaidi aaga dunia

Image
Emmanuel Makaidi Mwenyekiti wa chama cha siasa NLD, Dk Emmanuel Makaidi (74) amefariki dunia hii leo Oktoba 15, 2015  mchana katika hospitali ya Nyangao mkoani Lindi kwa kile kilichotaarifiwa kuwa ni shinikizo la damu. Kifo cha Makaidi kimethibitishwa na viongozi wa NLD ambao wanadai kupata taarifa kutoka kwa mjane wa marehemu, Modesta Ponera-Makaidi. Dk Makaidi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vya NLD, CHADEMA, CUF, na NCCR Mageuzi, pia alikuwa akiwania Ubunge wa Masasi Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Marehemu Dk Emmanuel Makaidi, mhandisi aliyebobea, alizaliwa Aprili 10, 1941 huko wilayani Masasi mkoani Mtwara. Baba yake mzazi alikuwa ni katekista wa Kanisa la Anglikana. Alianza elimu katika Shule ya Msingi Namalenga wilayani Masasi kati ya mwaka 1948 – 1952, mwaka 1953 – 1954 alisoma katika Shule ya Kati (Middle school) iitwayo Luatala hukohuko Masasi. Baaday...