DK MAGUFULI ASHIRIKI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU DK KIGODA DAR



 Mke wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Janeth Magufuli (kulia) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe.Mwantum Mahiza wakiwa wamemshikilia mke wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
 Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda, Omary Abdallah Kigoda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (kulia) akizungumza na Binti wa Marehemu Amina Kigoda ,katikati ni mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza.
Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimpa pole mke wa marehemu.


 Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. John Kijazi wakiwa kwenye mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda.
 Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati wa mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda.
 Mwili wa Marehemu Abdallah Kigoda ukipakiwa kwenye gari maalum mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
 Dada wa marehemu Abdallah Kigoda, Aisha Kigoda akiongozwa na ndugu na jamaa kuelekea nyumbani mara baada ya kuwasili wakitokea nchini India ambapo marehemu alikuwa akipata matibabu.
 Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na vyombo vya habari jinsi alivyomfahamu aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara, marehemu Dk Abdallah Kigoda wakati wa mapokezi ya mwili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA