JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI SIKU YA KUPIGA KURA
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari
jana (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na
viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba 25.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari
(hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na
viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila
shuruti wakati wa uchaguzi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Akizungumza
na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Mkuu wa Jeshi
hilo IGP Ernest Mangu amesema kuwa ulinzi utaimarishwa maeneo yote kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha
kuwa taifa linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu
na kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Ametoa
rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura siku hiyo bila wasiwasi wa aina
yoyote ili kuweza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
(Picha na Francis Dande)
(Picha na Francis Dande)
Comments
Post a Comment