Posts

MATOKEO CHAMPIONS LEAGUE, BARCELONA AIBUKA MSHINDI DHIDI YA ARSENAL HUKU JUVENTUS NA BAYERN NGOMA DRO

Image

Jaji wa mahakama ya juu asimamishwa kazi

Image
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi jaji wa mahakama ya juu aliyetuhumiwa kuchukua hongo katika kesi kuhusu kuchaguliwa kwa gavana wa Nairobi. Jaji Phillip Tunoi amesimamishwa kazi na Rais Kenyatta ameteua jopo la kuchunguza madai dhidi yake, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama. Jopo la kumchunguza jaji huyo litaongozwa na Jaji Sharad Rao ambaye ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Kuwachunguza Majaji na Mahakimu. Wanachama wengine wa jopo hilo ni Jaji Roselyn Korir,Jaji Mstaafu Jonathan Havelock,Judith Guserwa, James Kaberere Gachoka, Abdirashid Abdullahi Hussein na George Munji Wakukha. Jaji huyo anadaiwa kupokea rushwa kiasi cha shilingi $2m za Kenya ambapo yeye amekanusha madai dhidi yake. Chanzo BBC

Taarifa ya TBS kwa wazalisha nondo kuanza kuweka lebo / TBS steel bar ID & labelling

Image

MAGAZETI YA LEO JUMANNE, FEBRUARY 23

Image

Mjapan huyu aliyepo Tanzania kwa utafiti anaomba msaada baada ya kuibiwa

Image
Ujumbe ufuatao umepokelewa kupitia WhatsApp... Jana nikiwa Mombo nilimwona kijana mmoja wa kijapan amejibandika matangazo kifuani na mgongoni. Nilimwuliza kulikokoni akanieleza kuwa aliibiwa juzi vitu vyake ndani ya basi la Kidia one akisafiri kati ya dar Arusha. Kamera laptop na daftari 5 among other things. Vitu hivyo ni vina Research work aliyofanya miezi 6. Anaomba Msaada apate daftari zake. Na kama unavyoona yuko tayari kutoa 300,000/- Habari hii inatia uchungu sana. Tafadhali saidia kusambaza kwa makundi mengine huenda akafanikiwa. Tumemshauri pia aende clouds fm na media house zingine .

Maelekezo ya jinsi ya kuvuka kiusahihi taa za kuongozea barabara za makutano ya Morogoro Rd na Kawawa Rd

Image
 Comment Naomba nieleze kwa ufupi kuhusu matumizi ya barabara katika makutano ya barabara ya Morogoro/Kawawa eneo la Magomeni traffic lights. Nimeona nitoe ufafanuzi ili kusaidia uelewa kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo. Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa unapofika Magomeni traffic lights hauruhusiwi kupinda kulia (No right turn). Hivyo basi utaratibu upo kama ifuatavyo:- 1. Kwa madereva wanaotokea Jangwani kuelekea Kinondoni, atapaswa apitilize kama anaelekea Ubungo hadi kwa Shekhe Yahaya atapinda kulia na kurudi hadi Magomeni tragfic light na ndipo atapinda kushoto kuelekea Kinondoni (Kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na msikiti mkubwa kabla ya kufika traffic lights). Ama unapofika Magomeni Mapipa ukitokea Jangwani utapinda kulia na na kwenda kutokea eneo la Moroko hotel karibu na Kanisa la RC utapinda kulia kuelekea Kinondoni (kuna alama ya mchoro Barabarani eneo hilo la Mapipa inaelekeza kwenda kulia kwa wanaelekea upande huo). 2. ...

MAGAZETI YA LEO JUMATATU, JANUARY 22

Image
'