Jaji wa mahakama ya juu asimamishwa kazi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi jaji wa mahakama ya juu aliyetuhumiwa kuchukua hongo katika kesi kuhusu kuchaguliwa kwa gavana wa Nairobi.
Jaji Phillip Tunoi amesimamishwa kazi na Rais Kenyatta ameteua jopo la kuchunguza madai dhidi yake, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama.
Jopo la kumchunguza jaji huyo litaongozwa na Jaji Sharad Rao ambaye ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Kuwachunguza Majaji na Mahakimu.
Wanachama wengine wa jopo hilo ni Jaji Roselyn Korir,Jaji Mstaafu Jonathan Havelock,Judith Guserwa, James Kaberere Gachoka, Abdirashid Abdullahi Hussein na George Munji Wakukha.
Jaji huyo anadaiwa kupokea rushwa kiasi cha shilingi $2m za Kenya ambapo yeye amekanusha madai dhidi yake.
Chanzo BBC
Comments
Post a Comment