VIONGOZI WA AFRIKA WASHINDWA KUMCHAGUA MWENYEKITI MPYA WA TUME YA AU
Mkutano Mkuu wa viongozi wa Afrika jijini Kigali nchini Rwanda Viongozi wa mataifa ya Afrika wameshindwa kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja huo katika mkutano ya viongozi hao jijini Kigali nchini Rwanda. Hii inamaana kuwa Mwenyekiti wa sasa Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye alikuwa ametangaza kutowania tena wadhifa huo ataendelea kuongoza hadi mwezi Januari mwaka ujao wakati uchaguzi mwingine utakapofanyika. Msemaji wa Dlamini Zuma, Jacob Enoh Eben kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema baada ya mzunguko wa kwanza wa upigaji kura na kubainika kuwa hakuna mgombea aliyepata theluthi mbili ya kura ili kupata mshindi huku mataifa 28 kati ya 54 yakisusia zoezi hilo la kupiga kura. Kulikuwa na wagombea watatu, aliyekuwa Makamu wa rais wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Bostwana Pelonomi Venson-Moitoi na Agapito Mba Mokuy ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya Equatorial Guinea. Wiki iliyopita, kulikuwa na wasiwasi ikiwa...