WAZIRI MKUU AFUNGUA DUKA LA MSD WILAYANI RUANGWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya Wilaya ya Ruangwa akiwa katka ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.Kushoto kwake ni mkewe Mary na watano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa nakushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kukata utepe wakati akizindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Julai 16, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea duka hilo la MSD baada ya kulizindua kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majakipokea miguu miwili ya bandia kabla ya kuzindua duka la dawa la MSD lililokwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Julai 16, 2016. Miguu hiyo imetengeezwa na kutolewa msaada Kampuni ya Kamal Steel kwa wananchi wawili wa wilaya ya Ruangwa. Watatu kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia hospitali 524 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Akizindua duka hilo leo (Jumamosi, Julai 16, 2016) Waziri Mkuu amesema duka hilo litaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati katika wilaya ya Ruangwa pamoja na mikoa na wilaya za jirani. 

Duka hilo ni la sita kufunguliwa tangu Mhe. Rais Dk. John Magufuli alipotoa agizo kwa MSD kufungua duka la dawa ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo mengine yako katika mikoa ya Mwanza (Sekou Toure), Arusha (Mount Meru), Mbeya (karibu na hospitali ya mkoa) na Geita (hospitali ya wilaya ya Chato).

“Duka hili litasaidia kufikiwa kwa malengo ya Serikali ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wakati na kwa gharama nafuu, hivyo nawaomba mlitumie duka hili,” amesema. 

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa benki ya NMB, kikosi cha SUMA JKT na MSD kwa kufanikisha ujenzi wa duka hilo ambalo litaimarisha upatikanaji wa dawa kwa uharaka.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema kuanzishwa kwa duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa gharama nafuu , hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wa kwenda kuzitafuta katika ya mbali na kwa bei kubwa.

“Nitoe mfano wa tofauti wa bei za dawa kati ya maduka yetu na mengine, dawa ya sindano ya diclofenac tunauza sh. 250 huku mitaani ni sh. 1,000 hadi 1,500 , ampliclox dozi moja MSD sh. 1,500 mtaani sh. 3,500 na Ciprofloxacin MSD sh. 100 na mtaani sh. 500 hadi 1,000,” amesema. 

Mkurugenzi huyo amesema lengo la maduka hayo si kuuza dawa reja reja, nia yao ni kuziuzia hospitali, vituo vya afya na Zahanati ili wagonjwa wanapokwenda huko kupatiwa huduma wasikose dawa kwa wakati.

Akizungumzia kuhusu gharama za ujenzi wa duka hilo Bwanakunu mesema umegharimu sh.milioni 59 ambapo kati yake MSD imetoa sh. milioni 29 na benki ya NMB imetoa sh. milioni 30.“Mbali na gharama za ujenzi MSD tumenunua na kufunga vifaa vya TEHAMA kwa sh milioni 17 na mtaji wa dawa wa sh. milioni 37, ambapo imetenga sh. milioni 100 kwa ajili ya dawa za duka hilo.

Amesema duka hili litaendeshwa na kusimamiwa na MSD kwa muda wa mwaka mmoja na kisha wataikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya kuliendeleza ambapo litaisaidia katika kuiongezea mapato.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA