MAREKANI: POLISI WATATU WAUAWA KWA RISASI BATON ROUGE

media
Polisi yazuia barabara baada ya mauaji ya askari polisi katika mji wa Baton Rouge, mji mkuu wa jimbo la Louisiana, Julai 17, 2016.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vikinukuu ofisi ya meya, maafisa watatu wa polisi - ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa polisi na mwengine mwenye cheo cha juu - wameuawa kwa risasi katika mji wa Baton Rouge, katika jimbo la Louisiana.
Askari polisi angalau saba walikuwa wamelengwa kwa risasi. Katika mji huu, kifo cha kijana mmoja mweusi aliyeuawa kwa risasi na polisi mapema Julai mwaka huu kilizua wimbi la hasira na maandamano nchini Marekani hasa katika jimbo hilo la Louisiana.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha WAFB9, askari polisi wawili wameuawa lakini "angalau askari polisi 7 " walikuwa wamelengwa kwa risasi.
Televisheni ya taifa ya CBS imetaja idadi hiyo, ikimnukuu afisa mmoja wa polisi katika mji wa Baton Rouge.
askari polisi waliojeruhiwa wamesafirishwa hospitalini lakini hali inaonekana kudhibitiwa, kwa mujibu wa msemaji wa polisi katika mji wa Baton Rouge, Don Coppola.
Video iliyorushwa na kituo cha televisheni inaonyeshaaskari polisi wakiwasili katika eneo la tukio, huku kukisikika milio ya risasi.
Kwanza kunasikika mfululizo wa risasi kwa muda kadhaa na kisha muda mfupi milio midogo ya risasi.
Kwenye kituo cha televisheni ya WAFB9, mkuu wa mji wa Baton Rouge, Kip Holden amewataka raia kuwa watulivu, akihofia kutokea kwa machafuko mapya.
"Msikubali mtu yeyote kuchochea ghasia," Kip Holdem amesema.
Mji wa Baton Rouge, wiki za hivi karibuni, ulikumbwa na maandamano, ambayo kwa wakati fulani yalizimwa na polisi ikitumia nguvu za kupita kiasi. Maandamano hayo ya hasira yalifuatiwa na kifo, mapema mwezi Julai, cha Alton Sterling, Mmarekani mweusi aliyekua akiiuza bidhaa mbalimbali mitaani, ambaye alipigwa risasi na polisi.
Wiki iliyopita, polisi wa mji wa Baton Rouge ilisema kuwa liwakamata watu watatu ambao walikuwa na mpango wa mauaji ya askari polisi.
Mmoja ya watuhumiwa waliokamatwa, Antonio Thomas, mwenye umri wa miaka 17, alisema "wakati wa mahojiano yake kwamba yeye na watuhumiwa wengine watatu waliiba silaha na wangelitafuta risasi kwa minajili ya kuwashambulia polisi," taarifa kutoka polisi ilieleza Jumanne Julai 12.RFI

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA