Posts

VIONGOZI WA AFRIKA WASHINDWA KUMCHAGUA MWENYEKITI MPYA WA TUME YA AU

Image
Mkutano Mkuu wa viongozi wa Afrika jijini Kigali nchini Rwanda Viongozi wa mataifa ya Afrika wameshindwa kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja huo katika mkutano ya viongozi hao jijini Kigali nchini Rwanda. Hii inamaana kuwa Mwenyekiti wa sasa Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye alikuwa ametangaza kutowania tena wadhifa huo ataendelea kuongoza hadi mwezi Januari mwaka ujao wakati uchaguzi mwingine utakapofanyika. Msemaji wa Dlamini Zuma, Jacob Enoh Eben kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema baada ya mzunguko wa kwanza wa upigaji kura na kubainika kuwa hakuna mgombea aliyepata theluthi mbili ya kura ili kupata mshindi huku mataifa 28 kati ya 54 yakisusia zoezi hilo la kupiga kura. Kulikuwa na wagombea watatu, aliyekuwa Makamu wa rais wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Bostwana Pelonomi Venson-Moitoi na Agapito Mba Mokuy ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya Equatorial Guinea. Wiki iliyopita, kulikuwa na wasiwasi ikiwa...

ABIRIA WASHAMBULIWA KWENYE TRENI UJERUMANI

Image
Mshambuliaji aliuawa alipokuwa akikimbia baada ya kutekeleza tukio hilo Mtu mmoja aliyekuwa na Kisu na Shoka amewashambulia abiria waliokuwa kwenye Treni Kusini mwa Ujerumani usiku wa jumatatu na kuwajeruhi watu wanne kabla yeye kupigwa risasi na Polisi na kufa alipokuwa akikimbia baada ya tukio hilo. Polisi wa mjini Wuerzburg wameeleza kwenye ukurasa wao wa Facebook kuwa abiria watatu wamejeruhiwa vibaya na wengine 14 wanapata msaada wa kitabibu kutokana mshtuko walioupata. Polisi wamesema bado hakuna taarifa yeyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo. vyombo vya habari vya Ujerumani vimemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani mjini Bavaria kuwa mtu huyo ni mvulana wa miaka 17, mkimbizi mwenye asili ya Afghanistan. Mwaka jana Ujerumani iliwaandikisha wahamiaji milioni moja waliokuwa wakiingia nchini humo, zaidi ya 150,000 raia wa Afghanistan. Tangu mashambulizi ya hivi karibuni ya wanamgambo wa kiislamu nchini Ufaransa, kumekuwa na hali ya hofu ya kut...

MHADHIRI WA CHUO KIKUU-UDSM ANYAKUA TUZO NNE ZA FILAMU ZIFF 2016

Image
Bw.Amil Shivji akitangazwa kuwa mshindi tuzo kwenye tamasha la ZIFF baada ya filamu AISHA kutangazwa filamu bora Bw.Amil Shivji akipokea tuzo kwenye tamasha la ZIFF baada ya filamu AISHA kutangazwa filamu bora Usiku wa jana ulikuwa ni wa furaha ya aina yake kwa wadau mbalimbali waliokuwa wakiwania tuzo kwenye tamasha la kimataifa la filamu la ZIFF lililofanyika Zanzibar na miongoni mwa washindi hao ni Amil Shivji,ambaye pia ni mwalimu wa masuala ya uandaaji filamu kwenye idara ya sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Bw.Amil kupitia filamu ya AISHA iliyotengenezwa na kampuni ya Kijiweni Production kwa ushirikiano na shirika la Uzima kwa Sanaa(UZIKWASA) lilipo Tanga,kwa ujumla ilijishindia tuzo takriban nne katika kipengele kilichoshindanisha filamu za kiswahili, maarufu kama “bongo movie”. Filamu ya AISHA iliyotengenezwa Pangani-Tanga, imekwishachezwa kwenye zaidi ya matamasha thelathini(30) duniani, iliweza kuibuka kinara kwenye ZIFF kwa kutoa muongozaji bora(Omar Chan...

Kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya Tanzania leo Julai 18, 2016

Image

MAREKANI: POLISI WATATU WAUAWA KWA RISASI BATON ROUGE

Image
Polisi yazuia barabara baada ya mauaji ya askari polisi katika mji wa Baton Rouge, mji mkuu wa jimbo la Louisiana, Julai 17, 2016. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vikinukuu ofisi ya meya, maafisa watatu wa polisi - ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa polisi na mwengine mwenye cheo cha juu - wameuawa kwa risasi katika mji wa Baton Rouge, katika jimbo la Louisiana. Askari polisi angalau saba walikuwa wamelengwa kwa risasi. Katika mji huu, kifo cha kijana mmoja mweusi aliyeuawa kwa risasi na polisi mapema Julai mwaka huu kilizua wimbi la hasira na maandamano nchini Marekani hasa katika jimbo hilo la Louisiana. Kwa mujibu wa kituo cha habari cha WAFB9, askari polisi wawili wameuawa lakini "angalau askari polisi 7 " walikuwa wamelengwa kwa risasi. Televisheni ya taifa ya CBS imetaja idadi hiyo, ikimnukuu afisa mmoja wa polisi katika mji wa Baton Rouge. askari polisi waliojeruhiwa wamesafirishwa hospitalini lakini hali inaonekana kudhibitiwa, kwa mujibu wa msemaji w...

WAZIRI MKUU AFUNGUA DUKA LA MSD WILAYANI RUANGWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya Wilaya ya Ruangwa akiwa katka ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.Kushoto kwake ni mkewe Mary na watano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa nakushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kukata utepe wakati akizindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Julai 16, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea duka hilo la MSD baada ya kulizindua kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguz...

BODI YA NHIF YAUNDA MUUNDO MPYA WA WAKURUGENZI KUTOKA WAKURUGENZI TISA HADI WATANO

Image
Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani)   juu ya maboresho ya muundo wa safu ya wakurugenzi jana jijini, Dar es Salaa,Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani)  juu   ya hatua ya bodi waliochukua katika shirika hilo katika kubadili muundo wa wakurugenzi, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda. Wajumbe wa bodi na waandishi habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda.  ( picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii’) Na Chalila Kibbuda, Globu ya Jamii. BODI ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanya maboresho kwa kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka tisa hadi watano ili kuweza kufanya kazi kwa kasi katika utoaji  wa huduma kwa wananchi. Akizungumza na waandishi habari Makao Makuu NHIF leo  Mwenyek...