USIKU WA PUBLIC RELATIONS MANAGERS WAFANA SANA
Jana usiku ulikuwa ni usiku maalum sana kwa wanafunzi wanaosomea kozi ya Mahusiano ya umma na Masoko (PRO) wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino (SAUT)waliofanya sherehe yao pale Nyumbani hotel katika kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa Kwanza pamoja na kusherehekea ushindi wa FAWASCO (mshindi wa pili). Mgeni rasmi alikuwa ni mhadhili Emmanuel Silaa,pamoja na wageni wengine waalikwa kama Rais wa serikali ya wanafunzi (SAUTSO)Mh.Cosmas Mataba,akiambatana na waziri mkuu wake,pia na baadhi ya wahadhili kama Libelatus Chonya na Gibson.Sherehe iliambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa PR wenye vipaji mbalimbali. Mgeni rasmi mhadhili Emmanuel Silaa alitoa nasaa zake kwa wana PR kuwa wawe na ushirikiano wa kutosha kuanzia wanafunzi wa mwaka wa kwanza mpaka wa tatu na kuheshimiana hii itapelekea kukamilisha nguzo muhimu ya kozi hii unity and solidality hata watakapomaliza masomo yao na kuelekea kazin