Posts

VICHWA VYA MAGAZETI LEO ALHAMIS,DEC 13

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Mandela atibiwa ugonjwa wa mapafu

Image
Chapis Mzee Nelson Mandela Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela amepatwa tena na ugonjwa wa mapafu na anaendelea vyema na matibabu . Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94, amekuwa hospitalini mjini Pretoria tangu Jumamosi . Taarifa zinazohusiana Afrika Kusini Hii ni taarifa ya uhakika ya kwanza kutolewa kuhusu afya ya kiongozi huyo aliyepinga utawala ubaguzi wa rangi . Bw mandela alitibiwa mapafu miaka 2 iliyopita. Habari kuwa Mandelela anatibiwa ugonjwa wa mapafu, bila shaka imemaliza wasiwasi wa siku kadhaa kuhusu ukosefu wa taarifa zozote kuhusu afya yake Wananchi wa Afrika Kusini wanafuatilia kwa maakini taarifa za afya ya Mandela Msemaji wa rais huyo mstaafu hakueleza kuhusu ikiwa hali ya Mandela ni mbaya sana au itakuwa sawa lakini alisisitiza kuwa anaendelea kupokea matibabu. Miaka miwili iliyopita, hali kama hii ilijitokeza kuhusu Mandela baada ya kulazwa hospitalini kwa tatizo la kupum

Nguo fupi alias ‘vimini’ ni marufuku Vyuo vya KKKT

Habari imeandikwa na Yusuph Mussa -  Majira , Lushoto, Tanga MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo jijini Arusha, Profesa Joseph Parsalaw, amesema kuqanzia sasa ni marukufu kwa wanawake wanaosoma katika vyuo vikuu vyote na vile vishiriki vinavyomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kuvaa suruali za kubana au vimini. Prof. Parsalaw aliyasema hayo juzi katika mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), kilichopo Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga na kusisitiza kuwa, lengo ni kutoa wahitimu ambao watakubalika kwenye jamii kwa matendo yao pamoja na uvaaji wao. “Chuo Kikuu cha Tumaini kipo mstari wa mbele kuwahimiza wanafunzi na wafanyakazi kuzingatia maadili  anayokubalika kwenye jamii ya Kitanzania.  Hivi sasa katika vyuo vyote vishiriki, tumeweka bayana aina ya mavazi ambayo yanastahili kuvaliwa na vijana ili kudumisha heshima na maadili mema,” alisema Prof. Parsalaw. Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU, Mchungaji Dkt

VICHWA VYA MAGAZETI LEO JUMANNE DECEMBER 11

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .