Mandela atibiwa ugonjwa wa mapafu


Mzee Nelson Mandela
Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela amepatwa tena na ugonjwa wa mapafu na anaendelea vyema na matibabu .
Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94, amekuwa hospitalini mjini Pretoria tangu Jumamosi .
Hii ni taarifa ya uhakika ya kwanza kutolewa kuhusu afya ya kiongozi huyo aliyepinga utawala ubaguzi wa rangi . Bw mandela alitibiwa mapafu miaka 2 iliyopita.
Habari kuwa Mandelela anatibiwa ugonjwa wa mapafu, bila shaka imemaliza wasiwasi wa siku kadhaa kuhusu ukosefu wa taarifa zozote kuhusu afya yake
Wananchi wa Afrika Kusini wanafuatilia kwa maakini taarifa za afya ya Mandela
Msemaji wa rais huyo mstaafu hakueleza kuhusu ikiwa hali ya Mandela ni mbaya sana au itakuwa sawa lakini alisisitiza kuwa anaendelea kupokea matibabu.
Miaka miwili iliyopita, hali kama hii ilijitokeza kuhusu Mandela baada ya kulazwa hospitalini kwa tatizo la kupumua ingawa aliweza kutibiwa vyema.
Mandela pia alipokea matibabu ya kifua kikuu wakati alipokuwa gerezani, katika kisiwa cha Robben na afya yake, inaendelea kuwavutia watu wengi.
Mac Maharaj, msemaji wa rais, alisema kuwa wanajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kufahamisha watu,kuhusu afya yake lakini pia alitaka kutoingilia kazi ya madaktari pamoja na kutaka jamaa za Mandela kuruhusiwa kumzuru bila matatizo yoyote
source http://www.bbc.co.uk/swahili

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA