WASHIRIKI WA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK 2012 WATAJWA CHAGUA MWANAMITINDO NA MBUNIFU BORA 2012 Wandaaji wa Tuzo kubwa za mitindo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati wametangaza majina ya waliopendekezwa kushiriki katika kuwania tuzo mbalimbali za Swahili Fashion Week 2012 ikiwa pamoja na njia zitakazotumika kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo. Kufuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika tuzo za mwaka jana, Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zinazoendana na kusherehekea miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho hili kubwa la mitindo Afrika Mashariki na kati mwaka huu, zimeongezwa tuzo nyengine tatu kutoka katika tuzo za mwaka jana ili kuweza kutoa changamoto kubwa zaidi katika tasnia ya mitindo hapa nchini na ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati. Hivyo kufanya jumla ya tuzo 15 kuwaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana. Tuzo za mwaka huu ni: Best Male Model, Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year, East African Designer of the