TUZO KUBWA ZA MITINDO KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI ZA SWAHILI FASHION WEEK KUFANYIKA TENA KWA MARA YA PILI

WASHIRIKI WA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK 2012 WATAJWA
CHAGUA MWANAMITINDO NA MBUNIFU BORA 2012
Wandaaji wa Tuzo kubwa za mitindo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati wametangaza majina ya waliopendekezwa kushiriki katika kuwania tuzo mbalimbali za Swahili Fashion Week 2012 ikiwa pamoja na njia zitakazotumika kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo.
Kufuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika tuzo za mwaka jana, Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zinazoendana na kusherehekea miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho hili kubwa la mitindo Afrika Mashariki na kati mwaka huu, zimeongezwa tuzo nyengine tatu kutoka katika tuzo za mwaka jana ili kuweza kutoa changamoto kubwa zaidi katika tasnia ya mitindo hapa nchini na ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati. Hivyo kufanya jumla ya tuzo 15 kuwaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana.
Tuzo za mwaka huu ni: Best Male Model, Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year, East African Designer of the Year, Redd’s Stylish Female Personality, Stylish Male Personality, Innovative Designer, Best Men’s Wear, Fashion TV Program of the Year (Mpya), Vodacom Fashion Blog of the Year, Fashion Photographer of the Year, Fashion Journalist of the Year, Best East African Journalist (Mpya), Upcoming Designer.
Mchakato mzima wa kuchagua mwanamitindo na mbunifu wako bora kwa mwaka huu wa 2012 unasimamiwa na PUSH Mobile ambapo mpiga kura atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa Namba ya mshiriki (CODE) unaemkubali na kwenda kwenye namba 15678, huku mchakato mzima wa kuzihakiki kura hizo utafanywa na PKF. Lakini pia kura zinaweza kupigwa kupitia blogu maalum ya kupigia kura ya www.sfw2012awards.blogspot.com.
Washindi wote wa Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 watatangazwa siku ya ya mwisho ya Maonyesho ya Swahili Fashion Week, jumamosi ya tarehe 8, Desemba, 2012 katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es salaam, Tanzania.
Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka kati
Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na: Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security,  BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania),  Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century Cinemax and 361 Degrees.
Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka katika ukanda wa Afrika mashariki na kati kwa sasa. Huu ni mwaka wa Tano sasa, ambapo Swahili Fashion Week imekuwa ni Jukwaa la wanamitindo na watengeneza vito vya urembo kutoka katika nchi zinazoongea Kiswahili na bara zima la Afrika kwa ujumla kuweza kuonesha vipaji, kutangaza ubunifu wao na kukuza mtandao wa mawasiliano ya kibiashara ndani na nje ya nchi kwa wadau wa mitindo. Hili limelenga  kuhamasisha ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati  kwamba ubunifu wa mavazi ni njia moja wapo ya kujipatia kipato na wakati huo huo kukuza bidhaa zinazotengenezwa Afrika ( Made in Africa concept)

Ikiwa imeanzisha uhai na jukwaa la matumaini kwa kilinge cha mitindo katika ukanda huu, Swahili Fashion Week Swahili Fashion week imelenga kuwa maonyesho ya ubunifu wa mavazi linaloonekana sana Afrika na hasa kwa ajili ya soko la kimataifa, lililoundwa, kutengenezwa na kujengwa mwaka 2008 na Mustafa Hassanali.

Ifikapo mwaka 2013, Swahili Fashion Week ina lengo la kuwa ni tukio litakalotokea mara mbili kwa mwaka, ambapo kwa kuanza tukio la kwanza litafanyika nchini Kenya kama sehemu ya kwanza kisha tukio lenyewe kabisa kufanyika baadae nchini Tanzania kama sehemu ya pili.

Kwa Maelezo Zaidi:
BB Pin: 2380CDB6

Hassan Mrope
Public Relations and Communication Officer
361 DEGREES
PR | EVENTS | MEDIA
P.O.Box 10684, 105 Kilimani Road,
(Next to Embassy of France/Near NIDA Offices)
Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania.
Tel : +255 (0)22 266 8555
Mobile : +255 (0)713 441 892
Social Media : www.twitter.com/361tanzania
www.facebook.com/361TANZANIA
Web : www.361tanzania.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA