Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali. Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Sarah Reuben akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa Kikao kazi hicho mjini Dodoma. Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwasilisha mada kuhusu Mtazamo mpya wa Mawasiliano katika Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma. Mmiliki na muendeshaji wa mtandao wahabari