HII NI PAGE YA NECTA FAKE ILIYOPO FACEBOOK
Hii page feki ya NECTA ina watu zaidi ya elfu 11.
IMEKUWA IKITOA TAARIFA AMBAZO SIO ZA KWELI
Upotoshaji umeanzia kwenye page feki ya facebook ambayo inaendeshwa na watu wanaojifanya ni Necta, ni page ambayo imekua ikitoa habari za uongo kama unavyoiona hapo juu.
John Nchimbi msemaji wa NECTA amesema “matokeo ya kidato cha nne hayajatoka bado lakini yakiwa tayari Katibu Mtendaji ataita waandishi na yatawekwa kwenye mtandao wa NECTA, kuna watu wametoa hizo habari kwenye facebook na wanatumia nembo ya baraza la mitihani lakini NECTA hawana ukurasa wa facebook, hiyo taarifa sio ya ukweli na wala haina uhusiano wowote na baraza la mitihani, matokeo yatatoka kabla ya mwishoni mwa february 2013″
Comments
Post a Comment