Posts

DUDE: MWAKA 2014 NI GUNDU KWANGU

Image
Stori: Gladness Mallya TUKIWA tunaelekea ukingoni mwa mwaka, msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa mwaka 2014 ulikuwa hauna bahati (gundu) hivyo anamuomba Mungu huo ujao uwe wa baraka kwake. Msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’. Akipiga stori na gazeti hili, Dude alisema ndani ya mwaka huu hakuweza kufanikisha lengo lolote kati ya yale aliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa jambo ambalo linamuumiza kwani alitegemea kufanya mambo mengi lakini hakufanikisha. “Nilitegemea kufunga ndoa lakini imeshindikana kwa sababu upande wa kazi mambo hayakuwa mazuri pia nilipanga kwamba kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam kitarudi hewani lakini ikashindikana, ukweli mwaka huu haukuwa mzuri kabisa kwangu namuomba Mungu ujao akanifanikishe malengo yangu,” alisema Dude.

UNAIJUA AINA YA WATU WANAONYONYA NGUVU ZA WENGINE?

Image
Shukurani kwa Imani Ngwangwalu kwa kutushirikisha makala iliyopachikwa hapo chini. Mawasiliano yake yamepachikwa hapo mwishoni. Inaweza kuonekana kama ni kitu cha kushangaza lakini huu ndio ukweli wapo watu wanaonyonya nguvu za watu. Watu hawa wana uwezo wa kumwandama mtu hadi anakufa bila kujua. Watu hawa hawajafa,wako hai na tunaishi nao, wengine wakiwa ni watu wetu wa karibu sana, kama wazazi, wapenzi, watoto, jirani, marafiki au mabosi wetu. Hufanya vipi kunyonya nguvu zetu? Hutumia njia za aina mbalimbali, ambazo huzaa matunda kweli. Mtu anaweza kuuliza, inawezekana vipi mwingine anyonye nguvu zangu na hizo nguvu ni zipi? Kwa mfano, mimi ninapo kuwa nakukera kila siku, ninakugusa kihisia. Ninapokugusa kihisia, unaumia kihisia na kimwili. Baada ya muda Fulani wa kero zangu, nakuwa nimekupa athari kubwa kimwili na kiakili bila mwenyewe kujua na kama imeshawahi kukutokea umekerwa na mtu huwa inapelekea hata unapokutana na mtu huyu anayekukera

USIKU WA USWAZI NA WASWAZI NI NOMAAA DAR LIVE

Image
Msanii Inspector Haroun akiimba na mashabiki wake. Chid Benz kavua shati baada ya mzuka kumpanda.… Msanii Inspector Haroun akiimba na mashabiki wake. Chid Benz kavua shati baada ya mzuka kumpanda. Mesen Selekta akiimba kanyaboya pamoja na wacheza shoo. MC na Muimbaji, Pam D akizungusha nyonga. Mnyama, TID akiwa na kimwana stejini. Kundi la Umeme wakifanya yao stejini. Kala Pina akikumbushia ngoma za kitambo. Wabibi wakikamua. Kundi la Yakuza Mobb wakikamua. Wadau wa muziki wakiwa stejini. JANA katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar, wasanii kibao wamedondosha bonge la shoo katika Usiku wa Uswazi na Waswazi, shoo iliyoandaliwa na Defatality Music ikiwashirikisha mastaa wakongwe kama Chid Benz, Top in Dar ‘TID’ ,Yakuza Mobb, Kalapina, aka “Mbuge Mtarajiwa’’, Pam D pamoja na wasanii kibao wanaokuja kwa kasi wakiwemo Kundi la Umeme na Wabibi. Wasanii wengine waliodondosha

YANGA VS AZAM NGOMA DROO, WATOKA SARE YA 2-2

Image
Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Azam FC. Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akiwa kazini wakati wa mechi ya leo dhidi ya Azam FC. TIMU za Yanga na Azam FC leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye mtanange wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam yamewekwa kimiani na Didier Kavumbagu katika dakika ya 5… Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Azam FC. Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akiwa kazini wakati wa mechi ya leo dhidi ya Azam FC. TIMU za Yanga na Azam FC leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye mtanange wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam yame

NDEGE NYINGINE TENA YAPOTEA NI AIR ASIA

Image
  Bado dunia imebaki njia panda juu ya wapi ilipo ndege ya Malaysia Airlines 370 ambayo ilikuwa na abiria 239, ilipotea miezi zaidi ya nane iliyopita ikitokea Malaysia kwenda China, ndege nyingine imepotea, ilitokea Singapore kwenda Indonesia. Iliyopotea saa chache zilizopita ni AirAsia qz 8501,  ilikuwa na abiria 162 wengi wao walikuwa raia wa Indonesia na Uingereza imethibitisha kuwa kuna mtu mmoja raia wa nchi hiyo alikuwa akisafiri na mtoto wake. Ndege ilipotea wakati rubani alipolazimika kubadili mwelekeo wa ndege hiyo pasipo kuomba mwelekeo kutoka kwa waongozaji kutokana na hali mbaya ya hewa. Ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo wamejikusanya katika uwanja wa ndege wa Surabaya Indonesia , wakisubiri kupata taarifa yoyote itakayokuwa na matumaini kwao. Baadhi ya vikosi vinavyotafuta ndege hiyo vimesitisha zoezi hilo kutokana na hali mbaya ya hewa huku vingine vikiendelea.

50 CENT ACHUKIZWA NA TABIA YA ONGEZEKO LA MAUAJI YA WATU WEUSI MAREKANI

Image
Mwaka hauishi vizuri kwa Raia wa Marekani ambao wana asili ya Afrika, ile story ya ubaguzi ambayo huenda Dunia ilidhani imekwisha imechukua sura mpya kila kunapokucha, kinachosababisha story kuwa kubwa zaidi ni kitendo cha hali hiyo kujitokeza ndani ya Taifa la Marekani. Tumeona Marekani ikiwa mstari wa mbele kupambana na vingi, hii ishu ya ubaguzi wa rangi ni changamoto kubwa taifa hilo kwa sasa. Wameuawa wengi tayari ndani ya kipindi kifupi, watu hao wenye asili ya Afrika wameandamana na kutumia njia mbalimbali kuonyesha hawakuridhishwa na Mahakama kuwaachia huru Askari ambao wamefanya mauaji hayo. Kutokana na matukio hayo ya mauaji kuendelea kujitokeza rapper  50 Cent , ameamua kuvunja ukimya na kujitokeza kuelezea kukasirishwa kwake na matukio hayo ya mauaji na kupost picha ya  Hayati  Mahatma Gandhi  iliyoandikwa “ An eye for an eye makes the whole world blind “. Kisha akaandika ujumbe wa kuwafariji waliopata athari kutokana na tukio hilo; “ Condolences to the family

Idris Elba Ajibu Mashambulizi Ya Waliomponda Sababu Ya Rangi Yake baada ya kutengeneza movie na kuigiza kama James Bond

Image
Staa wa filamu ya The ‘Mandela: Long  Walk to Freedom   Idris Elba ametoa mtazamo wake kuhusu uvumi kuwa anatarajiwa kuchaguliwa kuigiza kama James Bond kwenye filamu za 007  zijazo. Kilichopeleka Idris kutoa mtazamo wake ni maneno mabaya ya ubaguzi yaliyotolewa na baaddhi ya mashabiki wa filamu hio kutoka Uingereza waliosema Idris ni mweusi ha wawezi kuwa James Bond kwa  sababu ya rangi yake. Kupitia twitter Idris ameandika “ Isn’t 007 supposed to handsome? Glad you think I’ve got a shot! Happy New year people, ” Twit ya Idris inamaana ”  Si 007 anatakiwa awe na mvuto ? nashukuru mnaodhani natakiwa kupata nafasi hii, heri ya mwaka mpya watu “ Limbaugh amesema  husika ya James Bond ilitengenezwa na  Ian Fleming kachero aliyefanya kazi  MI6 ya Uingereza na James Bond alikuwa mweupe na Mscottish . Aliendelea kusema  tumekuwa na James Bond weupe kwa miaka 50 sasa , nilazima awe Mscottish na awe anakunywa vodka iliyotingishwa na sio kukorogwa .

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI, DECEMBER 28 YAPO HAPA

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . .

GOOD NEWS: VANESSA MDEE ASHINDA TUZO NCHINI NIGERIA YA BEST FEMALE EAST AFRICA

Image
Kupitia ukurasa wake wa instagram, msanii wa muziki wa kizazi kipya na mtangazaji wa kituo cha Choice Fm,Vanessa Mdee aka V-Money kaandika "To God be the glory, Thank you soo much for voting. I love you"#BestFemaleEastAfrica #Tanzania amewashukuru mashabiki wake kuashiria ushindi huo alioupata katika kipengele cha Best Female EastAfrica nchini Nigeria kupitia tuzo za AFRIMA

NEW VIDEO: BONGE MOJA LA KICHUPA "SHAKE SHAKE" YA MSAMI

Naileta kwenu video mpya ya Msanii Msami inaitwa Shake Shake na imetayarishwa na kuongozwa na Aby Kaz

RATIBA YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA 2015 HII HAPA

Michuano ya ligi ya Mabingwa barani Afrika mwaka 2015 imepangwa kuanza kuchezwa Februari 13 mwaka 2015. Ratiba ya duru ya kwanza, mzunguko wa 16 wa fainali na mzunguko wa 8 ya michuano ya kifahari ya vilabu barani Afrika imepangwa ifuatavyo: Duru ya kwanza Mchuano wa kwanza  : Mbabane Swallows (Swaziland) vs Zesco (Zambia) Mchuano wa 2  : Séwé Sport (Côte d’Ivoire) vs AS Kaloum (Guinea) Mchuano wa 3  : USM Alger (Algeria) vs Foullah Edifice (Chad) Mchuano wa 4  : AS Pikine (Senegal) vs Etoile Filante Ouagadougou (Burkina Faso) Mchuano wa 5  : Al Hilal (Sudan) vs Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (Zanzibar) Mchuano wa 6  : Fomboni Club de Moheli (Comoro) vs Big Bullets (Malawi) Mchuano wa 7  : CD Libolo (Angola) vs SM Sanga Balende (DR Congo) Mchuano wa 8  : Kampala CC (Uganda) vs Cosmos de Bafia (Cameroon) Mchuano wa 9  : Azam (Tanzania) vs Al Merreikh (Sudan) Mchuano wa 10  : Lydia Ludic (Burundi) vs Kabuscorp (Angola) Mchuano wa 11  Sony de Ela Nguema (Equatorial Guinea) vs