TAARIFA YA MTATIRO KUHUSU KUKAMATWA KWA PROF: LIPUMBA
Prof. Lipumba akiwa katika gari la Polisi (picha: Habari Mseto blog) PROFESA LIPUMBA AKAMATWA NA POLISI KWA NGUVU! Ndugu zangu, hivi punde nimeongea na Maharagande Mbarala na Bonifasia Mapunda na wamenijulisha kuwa, Profesa Lipumba na Manaibu Wakurugenzi wawili wa Chama Cha Wananchi CUF (Shaweji Mketo na Abdul Kambaya), pamoja na walinzi wa Profesa Lipumba, wamekamatwa na polisi. Pia, nimeongea na mhe. Joram Bashange, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, tayari yuko Central Police lakini hajaruhusiwa kuwaona viongozi. Mawakili wa CUF wanaelekea polisi pia. KUMBUKIZI YA MWAKA 2001 Ukamataji huo uliotumia nguvu kubwa umetokea leo majira ya Mchana wilayani Temeke. Leo ni Januari 27 na ni siku yenye kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Wananchi CUF baada ya matukio ya mauaji yaliyofanyika tarehe na mwezi kama huu huko Zanzibar ambako wafuasi wa CUF zaidi ya 100 waliuawa kwa risasi na vyombo vya dola. Mauaji hayo yalifuatiwa na maandamano mbalimbali yakiwemo ya Dar Es Salaam yaliyoongozwa na Pro