AJALI YA MOTO KICHANGA CHAOKOA FAMILIA!


Na Gabriel Ng’osha/Risasi Mchanganyiko
KICHANGA kinachokadiriwa kuwa na umri wa miezi nane, wiki iliyopita kiliiokoa familia yake kuteketea kwa moto, baada ya kuamka usiku na kulilia kunyonya, kitendo kilichomshtua mama yake aliyebaini nyumba yao ilikuwa ikiungua, huko Kibamba Lungwe jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya nyumba iliyoungua.
Akisimulia tukio hilo, mama wa kichanga hicho, Asha Mohamed, alisema alishtuka baada ya mtoto kuanza kulia akitaka kunyonya, alipoamka ndipo akaona mwanga mkali juu ya paa, hali iliyomlazimu kuamka na kwenda kumgongea Abuu ili kutafuta njia ya kutoka,” alisema mama huyo akiongeza kuwa sebuleni, moto ulikuwa umetapakaa.
Kijana Abuu Masoud (15), baada ya kuamshwa, alionyesha ujasiri na upendo mkubwa kwa kujitoa mhanga kuwasaidia wadogo zake watatu waliokuwa wamelala katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo.
Baada ya kuingia katika chumba hicho, alifanikiwa kumtoa mtoto mmoja.
Watoto walionusulika kuteketea kwa moto.
“Nilipofungua mlango wa sebuleni nikaona moto na moshi mwingi sana, roho iliniuma sana kwani chumba cha pili kulikuwa na wadogo zangu watatu wamelala, nikaamua  kuvaa ujasiri na kujitosa  katika chumba kile na kufanikiwa kutoka na mtoto mmoja, wakabaki wawili,
baada ya kurudi ndani nikapata wazo la kuzima Mean switch, nilipoenda kuishika ikaniangukia kichwani kwani ilikuwa imeshaungua, ndiyo nikaungua na kushindwa kuwatoa waliobakia, ingawa baadaye kuna msamaria mwema mmoja alijitokeza na kuja kubomoa mlango na kuwatoa wengine,” alisema kijana huyo.
....Kitanda walichokuwa wamelala.
Mama wa mtoto mchanga alifanikiwa kutoka pasipo kudhurika.
Aidha baba mwenye nyumba hiyo, Khalfani Maketemo, ambaye wakati nyumba yake inaungua yeye na mkewe walikuwa hospitali alikokuwa amelazwa, anadai chanzo cha moto huo ni shoti iliyoanzia kwenye bati na anaamini  ni kutokana na kuunganishwa vibaya kwa waya unaopitisha umeme kutoka kwenye nguzo kwenda kwenye nyumba.
Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya majirani walisema; “Uunganishwaji wa umeme ni wa kubabaisha, waya unagusana na bati jambo  ambalo ni hatari kama waya utachubuka na mvua kunyesha’’.Familia hiyo kwa sasa haina sehemu ya kujisitiri nyumba nzima imeteketea.
Kujua mengi tembelea www.globaltvtz.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA