WASTARA AKIRI KUSHUKA KISANAA BAADA YA KUFARIKI SAJUKI


Stori: Mayasa Mariwata/Risasi Mchanganyiko 
STAA wa filamu nchini, Wastara Juma amesema anajihisi kupoteza mwelekeo unaomfanya kushuka kisanaa tokea kufariki kwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kwani ari yake ya kufanya kazi imepotea.
Staa wa filamu nchini, Wastara Juma.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, alisema Sajuki alikuwa ni msaada mkubwa sana kwake kisanaa mbali na maisha ya kawaida, kwani anashindwa kupita njia alizokuwa anapitishwa na mumewe huyo kiasi cha kujikuta akitoa filamu kati ya mbili hadi tatu kwa mwaka.
“Nikiri tu kwamba nimeshuka kisanaa, kasi ya kipindi kile imepungua, mume wangu alikuwa akijituma kuhakikisha mikakati yetu inaenda, kwa mwaka mzima nilitoa filamu hata tatu lakini toka asa naambulia moja tu mwaka mzima,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA