Posts

BURUDANI MGANGA WA DIAMOND JELA MIAKA 7, HAKIMU ASOMA HUKUMU KIJASHO KIKIMTOKA!

Image
Yule mganga aliyejitapa kumtengenezea nyota ya mvuto staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya amehukumiwa kifungo cha miaka saba (7) jela baada ya kukutwa na hatia katika kisa cha kuchanganya akihusishwa na wizi wa gari. Ustadh Yahya akiwa chini ya ulinzi. TUJIUNGE MAHAKAMA YA WILAYA YA ILALA Habari za uhakika zilieleza kwamba aliyehitimisha kesi hiyo ni Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar, Hassan Kisailo mapema Jumatatu wiki hii wakati jua la asubuhi likiwaka. HAKIMU ASHUSHA MIWANI Huku kijasho chembamba kikimtiririka huku akishusha miwani kidogo kuona wahudhuriaji wa kesi hiyo, Hakimu Kisailo alitoa hukumu hiyo kwa maelezo kwamba, mnamo Januari 20, mwaka jana, maeneo ya Kariakoo jijini Dar, Yahya alidaiwa kuiba gari aina ya Toyota RAV4 lenye namba za usajili T 139 BSJ likiwa na thamani ya Sh. milioni 12, mali ya Edrick Elieza. Wakati Hakimu Kisailo akisoma hukumu hiyo, mshtakiwa na wadhamini wake hawakuwepo maha

JANGA TENA: NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA, DAR

Image
Nyumba iliyoteketea kwa moto. Mashuhuda wa tukio wakitazama nyumba iliyoungua.… Nyumba iliyoteketea kwa moto. Mashuhuda wa tukio wakitazama nyumba iliyoungua. Mmoja wa wanafamilia wa nyumba hiyo, Abdallah Mohamed akiwa katikati ya vyumba vilivyoungua. Baadhi ya vitu vilivyookolewa vikiwa nje ya nyumba hiyo. NYUMBA  moja iliyopo maeneo ya Mwananyamala ‘B’ shuleni,  mali ya Bi. Zena Abdallah imeteketea kwa moto jioni hii. Hili ni tukio la pili la moto kuunguza nyumba siku ya leo jijini Dar es salaam baada ya moto mwingine kuteketeza Club Olympia mapema leo! Chanzo cha kuungua moto nyumba hiyo inadaiwa ni hitilafu ya umeme uliokuwa ukikatika na kuzima. Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamedai kuwa huenda hitilafu hiyo imetokana na matengenezo ya Tanesco yaliyokuwa yakiendelea kwani chanzo cha hitilafu hiyo  kilianzia upande wa  mita ya umeme  wa nyumba hiyo. (HABARI/PICHA:  DENIS MTIMA/GPL)

SIMBA YACHAPWA NA MBEYA CITY TAIFA

Image
Simba SC wakimenyana na Mbeya City katika Uwanja wa Taifa jijini Dar. (Picha na Maktaba Yetu) SIMBA SC imeendelea kupoteza michezo yake hasa ya nyumbani baada ya leo kukubali tena kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City. Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imepigwa muda mfupi uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba hivi karibuni ilipoteza mechi yake ya nyumbani baada ya kupigwa na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC… Simba SC wakimenyana na Mbeya City katika Uwanja wa Taifa jijini Dar. (Picha na Maktaba Yetu) SIMBA SC imeendelea kupoteza michezo yake hasa ya nyumbani baada ya leo kukubali tena kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City. Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imepigwa muda mfupi uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba hivi karibuni ilipoteza mechi yake ya nyumbani baada ya kupigwa na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya kutoka sare ya bao

WAZAZI WA MANAIKI WAMTOLEA NJE WOLPER

Image
Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga,amesema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwa sababu wazazi wake wamemtolee nje ishu ya kwenda kumposa staa wa kike Bongo, Jacqueline Wolper. Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga akiwa na Jacqueline Wolper. Akizungumza kwa masikitiko, Manaiki alisema kuwa hivi karibuni alifunga safari na kwenda kijijini kwao Mbeya kwa ajili ya kuwaeleza wazazi wake nia yake ya kumuoa Wolper lakini imekuwa tofauti kwani wamemwambia kama anataka kuoa msichana atatoka nyumbani kwao. “Yaani nimeamini kabisa mbio za sakafuni huishia ukingoni, sikujua kama wazazi wangu watanikata maini kwa kuwa nilijua wazi hawatakuwa na kipingamizi lakini wameniambia kuwa lazima nioe nyumbani,” alisema.

KLABU OLYMPIA IMETEKETEA KWA MOTO

Image
Klabu Olympia iliyopo Mori- Sinza jijini Dar Es Salaam imeteketea kwa moto leo alfajiri chanzo chake kikidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme. Jitihada za kuzima moto huo zinaendelea. Habari zaidi kuwajia baadae.