JANGA TENA: NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA, DAR

Nyumba iliyoteketea kwa moto.
Mashuhuda wa tukio wakitazama nyumba iliyoungua.…
Nyumba iliyoteketea kwa moto.
Mashuhuda wa tukio wakitazama nyumba iliyoungua.
Mmoja wa wanafamilia wa nyumba hiyo, Abdallah Mohamed akiwa katikati ya vyumba vilivyoungua.
Baadhi ya vitu vilivyookolewa vikiwa nje ya nyumba hiyo.
NYUMBA moja iliyopo maeneo ya Mwananyamala ‘B’ shuleni,  mali ya Bi. Zena Abdallah imeteketea kwa moto jioni hii. Hili ni tukio la pili la moto kuunguza nyumba siku ya leo jijini Dar es salaam baada ya moto mwingine kuteketeza Club Olympia mapema leo!
Chanzo cha kuungua moto nyumba hiyo inadaiwa ni hitilafu ya umeme uliokuwa ukikatika na kuzima. Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamedai kuwa huenda hitilafu hiyo imetokana na matengenezo ya Tanesco yaliyokuwa yakiendelea kwani chanzo cha hitilafu hiyo  kilianzia upande wa  mita ya umeme  wa nyumba hiyo.
(HABARI/PICHA:  DENIS MTIMA/GPL)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA