MAMBO 10 ALIYOZUNGUMZA LOWASSA NA WAANDISHI WA HABARI KWA MARA YA KWANZA
Mhe. Edward Lowassa amefanya mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma ambapo ananukuliwa kusema yafuatayo kwa muhtasari: 1. Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii. 2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa ni waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo Aliekuwa DC Igunga Elibariki Kingu. Pia aliyekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki naye alikuwepo. Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo gani na kwan