WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila. MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino). Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso Kalonge (wakazi wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje), na Leonard Msalage Mwakisole na Hakimu Mselem Mwakalinga (wakazi wa Kiwira wilayani Rungwe). Mshtakiwa wa nne, Mawazo Philemon Figomole, ameachiliwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasi na shaka kwamba alihusika katika mauaji hayo. Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya mauaji yenye kumbukumbu Namb. KIW/IR/49/2008 na PI 5/2013, Jaji wa Mahakama Kuu Dk. Revila, amesema mahakama imejiridhisha pasi