Orodha ya majina ya waliochaguliwa kujiugna Kidato cha Tano
Kuna faili limepachikwa hapo chini au
- Fungua linki ifuatayo kutafuta majibu hayo: pmoralg.go.tz/selection
au
- Fungua linki ifuatayo yenye faili (pdf) lenye orodha hiyo: pmoralg.go.tz....pdf
TAARIFA KWA UMMA
OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana 31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 na wavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 na wavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa na fursa ya mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI ya www.pmoralg.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OWM-TAMISEMI
Comments
Post a Comment