37 WAUAWA KWA AJALI YA NDEGE INDONESIA

Umati wa watu ukishuhudia ajali hiyo.Vikosi vya usalama vikiwa kazini.Sehemu ya mabaki ya ndege hiyo.Shughuli za uokoaji zikiendelea katika eneo la tukio.
JAKARTA, Indonesia
NDEGE ya Uchukuzi ya Jeshi la Anga la nchini Indonesia imeanguka eneo la Medan, Kaskazini mwa Jimbo la Sumatra mapema leo.
Maofisa wa jeshi la nchi hiyo wamesema kuwa, tayari miili 20 ya watu waliokufa kwa ajali hiyo imepatikana katika eneo la ajali.
Maofisa hao wameongeza kuwa, ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya C-130 Hercules ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 50 wakati ilipoanguka.
Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.
Ndege hiyo iliharibu nyumba baada ya kuanguka katika mji wa Medan, kaskazini mwa Jimbo la Sumatra.
Picha za runinga zilizorekodiwa wakati ndege hiyo ilipokuwa ikianguka na zile za kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Anga nchini Indonesia amesema kuwa, rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.
CREDIT: BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA