Posts

JK AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan BAntu a

MAGAZETI YA JUMANNE, SEPTEMBER 8

Image

#TEAM EMPIRE, MSIMU MPYA KUZINDULIWA SEPTEMBER 23,WAACHIA SOUNDTRACK 2

Image
Empire Msimu wa pili uko njiani mtu wangu, tunahesabu siku chache kufikia tarehe 23 September ili tuweze kuenjoy ile series iliyoshika headlines kubwa sana duniani! Kama wewe ni shabiki mkubwa wa Empire basi hii good news ikufikie, soundtrack 2 mpya za Empire zimetoka, hapa nazungumizia ‘No Doubt About It’ iliyomshirikisha Pitbul na Jussie Smollett anayeigiza kama (Jamal Lyon) wimbo huu umeandikwa na Ne-yo. Nyingine ni ‘All About The Money’ ndani anasikika Yazz The Greatest ambae anacheza kama Hakeem Lyon kwenye Series ya Empire.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBER 6 YAPO HAPA

Image

UKAWA Mbarali waungana na ACT-Wazalendo kwa ajili ya Ubunge tu

Wapiga kura huko Mbarali wameamua kuungana na kuunda umoja wao kwa ajili ya kushinda kiti cha Ubunge tu, ili jimbo libaki kwa Modestus Kilufi, mgombea kutoka ACT-Wazalendo. Wakizindua kampeni zao, wamesema wameamua kufanya hivyo baada ya UKAWA (CHADEMA, CUF, DP na NCCR-Mageuzi) kushindwa kupata mgombea mmoja anayekubalika na vyama vyote vinavyounda umoja huo. Kilufi ni nani? Bofya hapa  na pia hapa ili usome kwa ufupi taarifa ziliyotangulia kumhusu.

Rashid Mwishehe “Kingwendu” anadiwa kwa Ubunge Kisarawe

Image
Umati wa watu ukiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Majengo wilayani Bagamoyo.i uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kisarawe mkoa wa Pwani. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed (kulia) akiteta jambo na mgombea wa jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu” Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kisarawe katika mkutano wa kampeni. Mgombea ubunge jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu” akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni.  (P.T) Juma Duni Haji akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Kisarawe, Rashid Mw

Uchina yafaa kueleza sera zake za uchumi

Image
Wizara ya fedha ya Marekani imesema inaonesha Uchina imefahamu kwamba inahitaji kuimarisha mawasiliano kuhusu sera zake za uchumi baada ya mtafaruku wa mwezi uliopita katika masoko ya fedha ya kimataifa. Taarifa hiyo inafuatia mazungumzo baina ya waziri wa fedha wa Marekani, Jack Lew, na mwenzake wa Uchina, Lou Jiwei, kando ya mkutano wa mataifa 20 yenye uchumi mkubwa kabisa duniani - G20. Bwana Lew piya aliisihi Uchina isipunguze thamani ya sarafu yake, ili kufanya bidhaa inazosafirisha nje kuwa rahisi. Mazungumzo hayo yanayofanywa Ankara, Uturuki, yaliangalia haja ya kukuza uchumi na kuzidisha imani katika masoko baada ya bei za hisa kuporomoka mwezi uliopita, huko Uchina na sehemu nyingi za dunia. BBC