Uchina yafaa kueleza sera zake za uchumi
Wizara ya
fedha ya Marekani imesema inaonesha Uchina imefahamu kwamba inahitaji
kuimarisha mawasiliano kuhusu sera zake za uchumi baada ya mtafaruku wa
mwezi uliopita katika masoko ya fedha ya kimataifa.
Taarifa
hiyo inafuatia mazungumzo baina ya waziri wa fedha wa Marekani, Jack
Lew, na mwenzake wa Uchina, Lou Jiwei, kando ya mkutano wa mataifa 20
yenye uchumi mkubwa kabisa duniani - G20.
Bwana Lew piya aliisihi Uchina isipunguze thamani ya sarafu yake, ili kufanya bidhaa inazosafirisha nje kuwa rahisi.
Mazungumzo
hayo yanayofanywa Ankara, Uturuki, yaliangalia haja ya kukuza uchumi na
kuzidisha imani katika masoko baada ya bei za hisa kuporomoka mwezi
uliopita, huko Uchina na sehemu nyingi za dunia.BBC
Comments
Post a Comment