LOWASSA AENDELEA NA ZIARA ZAKE ZA KAMPENI, BARIADI MKOANI SIMIYU
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA wa Mkoa wa Simiyu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia