Posts

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa uamuzi wa Serikali kuhusu Serikali kuhusu Tiba Asili  na Tiba Mbadala katika mkutano wa  waandishi  ulifanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. kushoto ni  Naibu Waziri wa Wizara hiyo, DK. Hamis Kigwangalla wakifuatilia tukio hilo. Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigangwalla akifafanua jambo kuhusu uamuzi wa  Serikali kuhusu Tiba Asili  na TibaMbadala katika mkutano wa  waandishi  ulifanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. kushoto ni  Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu.

Taarifa ya hatua ya TMAA dhidi ya waliotorosha, na biashara haramu ya madini

Image
UDHIBITI WA UTOROSHAJI NA BIASHARA HARAMU YA MADINI  Moja ya majukumu ya Wakala wa Ukaguzi wa madini Tanzania (TMAA) ni kufuatilia na kuzuia utoroshaji/magendo na biashara ya madini unaopelekea ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kushirikiana na taasisi nyingine husika za Serikali zikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya Uhamiaji.  Taarifa za matukio ya udhibiti wa utoroshaji na biashara haramu ya madini zilizopo zinaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2015 mpaka Januari 13, 2016 kulikuwepo na jumla ya matukio 14 ya utoroshaji wa madini ambapo madini yenye thamani ya Dola za Marekani 1,474,194 milioni (zaidi ya Shilingi bilioni 3,235,856,181) yalikamatwa na wakaguzi wa Wakala kupitia Madawati ya Ukaguzi yaliyopo katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Mwanza.  Katika matukio ya hivi karibuni ya ukamataji wa madini katika viwanja vya ndege, madi

NAIBU WAZIRI ATEMBELEA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

Image
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni (kushoto), akiongozana  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Dickson Maimu (kulia), wakati wa ziara ya kutembelea moja ya ofisi za mamlaka hiyo,iliyopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi,jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri aliweza kupata fursa ya kuangalia jinsi utengenezaji wa kitambulisho cha Utaifa unavyofanyika. Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni, akiwa katika kikao na viongozi mbalimbali wa Vitengo vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),wakati wa ziara iliyoanzia Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dickson Maimu. Afisa Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Emmanuel Joshua(kushoto), akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni(katikati),wakati wa ziara ya Naibu Waziri kwe

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI, JANUARY 16

Image

AIRTEL YAZINDUA DUKA LA KISASA JIJINI DAR

Image
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(wakwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja Bi. Zakia Omary Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi. Beatrice Singano Mallya . Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald (kulia) akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng. Edwin Ngonyani juu ya hu

Wafanyakazi wageni 15 wa mgodi wa Tanzanite One wafukuzwa nchini

Image
Teresia Mhagama na Mohamed Saif Jumla ya raia wa kigeni 15 waliobanika kufanya kazi kinyume na taratibu za kisheria katika mgodi wa Tanzanite One uliopo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wameondoshwa nchini tarehe 25 Desemba, mwaka jana. Hayo yalielezwa jana jijini Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Amos Makala wakati wa kikao chake na wajumbe wa kamati hizo pamoja na Naibu Katika Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe kilichofanyika katika Kituo cha Jimolojia jijini humo. Alisema kuwa raia hao waliamuliwa kuondoka nchini na Idara ya Uhamiaji mkoani Manyara ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa hiyo ambazo ziliunda kikosi kazi cha wajumbe 13 kwa ajili ya udhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite nje ya nchi, ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni zinazoshughulika na biashara ya madini na kuchunguza raia wa kigeni wasiokuwa na sifa za

MAGAZETI YA LEO IJUMAA, JANUARY 15

Image