Posts

Polisi yazima ghasia iliyozuka kati ya Wamasai na Watatoga wa Simanjiro na Kondoa

Image
Info Post Subi Nukta 2/18/2016 12:01:00 AM No Comment

TTCL yakanusha taarifa za mfumo wake wa mawasiliano kuingiliwa na kudukuliwa

Image
Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka akifafanua jambo kwenye mkutano na vyombo vya habari leo. KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni hiyo umeingiliwa na wadukuzi. Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Nicodemus Thomas Mushi alisema taarifa zinazotolewa si za kweli hivyo kuwataka wateja wao wazipuuze. “...Tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi, na kwamba mifumo yetu ya Mawasiliano ya TTCL ipo salama, huduma zetu zote zipo thabiti na mpaka sasa tunapotoa taarifa hii, hakuna uhalifu wowote uliofanyika kwa sisi wenyewe kama Kampuni wala kwa mteja wetu yeyote,” alisema Thomas Mushi. Aidha, tunapenda kuwathibitishia kuwa, taarifa za Wateja wetu wote ikiwemo Serikali , Idara, Wakala na Taasisi za Umma, Taasisi za fedha, M

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI, FEBRUARY 18

Image

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AAGWA RASMI SHULE YA MSINGI MBUYUNI

Image
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ameketi kwenye meza yake katika ofisi ya waalimu katika shule ya Msingi ya Mbuyuni jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

TAARIFA KUTOKA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015

Image
Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016.  Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki. Hivyo, Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara haijasitisha utoaji wa matokeo hayo. Matokeo yatatangazwa mara tu mchakato utakapokamilika.  Imetolewa na,  AFISA HABARI NA UHUSIANO  TAARIFA NECTA

MAENDELEO YA UJENZI WA BOMBA LA MAJI RUVU CHINI, PWANI - DAR ES SALAAM

Image
Mafundi wakiendelea na kazi ya kulaza mabomba ya Maji eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam. Mabomba hayo ambayo sasa yamekamilika kwa urefu wa kilometa 54.8 kati ya 55.9 yatatumika kusafirisha maji kutoka mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Maneja wa Kampuni ya Gauff Consultants, Thorsten Seitz akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa bomba hilo la kusafirishia Maji kutoka Ruvu Chini Chanzo:wavuti.com

WAZIRI NDALICHAKO ASITISHA MKATABA WA MKURUGENZI BODI YA MIKOPO NA KUSIMAMISHA WAKURUGENZI 3 HESLB

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amevunja mkataba wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) nchini, George Nyategi na kuwasimamisha kazi wakurugenzi wengine watatu huku akitaka uchunguzi ufanyike haraka. Mkataba wa Bw. Nyageti uliopaswa kuisha tarehe 31/08/2016 umevunjwa leo na kuamriwa alipwe mshahara wa mwezi mmoja kwa mujibu wa kifungu namba 50,03,a cha kanuni za kudumu. Wengine waliokumbwa na fagio hilo ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Yusuph Kisare, Juma Chagonja, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo na Bw. Onesmo Laizer na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo, Yusuf Kisare. Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuwepo kwa ukiukwaji wa utoaji wa mikopo pamoja na ucheleweshaji usio na sababu za msingi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Profesa Ndalichako amesema kuwa bodi ya mikopo imekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wanafunzi wanaostahili kupata mikopo na kufanya kwao kuweza