RIPOTI: USHINDI WA TRUMP NI HATARI KWA DUNIA
Trump anaongoza miongoni mwa wagombea wa Republican Shirika moja la kimataifa limesema ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa miongoni mwa hatari 10 kuu zaidi zinazokabili dunia. Shirika hilo la Economist Intelligence Unit linaonya kuwa iwapo Bw Trump atashinda urais Marekani, hilo huenda likavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani. Hata hivyo, shirika hilo halimtarajii Bw Trump, anayeongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican, kumshinda Bi Hillary Clinton ambaye shirika hilo linasema "ana uwezekano mkubwa sana kuwa mgombea wa chama cha Democratic". Ushindi wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya kivita katika bahari ya South China Sea. Kuyumba kwa uchumi wa Uchina au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na kusababisha “vita baridi” vipya ni miongoni mwa mambo ambayo yanac