Monduli yamzuia mwekezaji kuendelea kujenga hotali mlimani

Info Pos
Hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha imesitisha ujenzi wa hoteli ya kitalii ya mwekezaji raia wa Uholanzi, Menno Hofland juu ya Mlima Losimingori.

Akihutubia wakazi wa Kijiji cha Losirwa juzi, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Ephraem Ole Nguyaine alisema hatua hiyo inafuatia malalamiko ya wakazi hao yaliyoripotiwa na gazeti hili hivi karibuni kupinga umiliki wa ardhi kwa mwekezaji huyo.

Wakazi hao wamekuwa wakimlalamikia mwekezaji huyo kuhodhi ardhi ya kijiji zaidi ya ekari 120 kinyume cha taratibu na kwamba, amekuwa akiwafukuza kwa silaha wanapopeleka mifugo eneo hilo kwa ajili ya malisho.

Hata hivyo, Hofland alieleza kuwa eneo hilo ameuziwa na mfugaji, Kimeshwa Kipailel kwa kufuata taratibu zote za kijiji na kwamba awali aliuziwa ekari 50 na baadaye kuongeza 70 juu ya mlima.

Kipailel alisema hajauza eneo hilo bali amempatia hekari 50 mwekezaji huyo kujenga hoteli kwani makubaliano ni kuwa watakuwa wakigawana faida.

“Mimempa ni eneo langu ajenge hoteli, ikikamilika atakuwa ananipatia asilimia ya fedha ambazo watalipa wageni,” alisema

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Masiyaya Kimiti alisema Serikali yake haitambui umiliki wa eneo hilo kwa mwekezaji huyo.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA